Tuesday, July 26, 2011

MAPENZI: Mwanamke, ULIPENDEWA NINI?

Katika makala iliyopita, nilijaribu kuelezea tabia moja ya wanaume katika mahusiano ambayo hujitokeza mara nyingi, na wakati mwingine, pande zinazohusika zinakuwa hazielewi ni kwa nini hali kama hiyo huweza kutokea na namna ya kuchukuliana nayo pale inapokuwa imejitokeza.

Kabla sijaendelea pia, napenda kuelezea kuwa makala hizi zinalenga zaidi kutoa “sauti ya wanaume” katika masuala ya mahusiano. By “sauti ya wanaume” simaanishi kwamba mimi ndimi msemaji wa wanaume, bali najaribu kuelezea masuala mbalimbali ya wanaume katika mahusiano, ambayo mara nyingi huwa hayafahamiki au kueleweka vizuri kutokana na sababu mbalimbali.

Katika makala ya leo, nitajikita zaidi katika kujadili KIINI CHA KUPENDWA katika kuimarisha na kudumisha mahusiano. Kwanza kabisa, ni muhimu kufahamu kuwa kila palipo na mapenzi/mahusiano ya kimapenzi kati ya watu wawili huwa kunakuwa na sababu iliyowaleta pamoja hao watu hadi wakaingia katika hayo mahusiano. Kwa upande wa wanaume, baadhi ya sababu za kumpenda na kumchagua msichana huwa ni pamoja na Uzuri wa Sura, Umbile la Mwili, Saizi ya Mwili (mnene/mwembamba), rangi ya ngozi, kimo, upeo wa ufahamu, elimu, dini, kabila n.k. n.k.

Makala hii hailengi katika kuangalia msingi/uhalali wa ‘vigezo’ hivyo kwa undani, bali umuhimu wa ‘vigezo’ hivyo katika kuyadumisha na kuyaendeleza mapenzi hayo.

Kwako mwanamnke unayependwa na mwanamne, moja ya mambo ya muhimu sana kwako kuyaelewa ni sababu ya huyo mwanamme kukupenda wewe. Ni muhimu sana kuelewa ni kitu gani kilichomfanya akawavuka wasichana wengine wote aliokutana nao maishani mwake tangu akiwa mtoto hadi akaamua kukuchagua wewe. Umuhimu wa kuelewa sababu hizo unatokana na umuhimu wa vigezo hivyo katika kuendeleza au kukatisha uhusiano wenu huko mbeleni.

Namna za Kuweza kufahamu

Kuna njia nyingi ambazo unaweza kuzitumia kuweza kuupata ukweli kutoka kwa mwenzako kuhusu sababu za yeye kukupenda. Hakuna njia ambayo ni ya uhakika kuweza kukupatia majibu kamili na unayoyahitaji, hivyo ni muhimu kufaham na kutumia njia mbalimbali. Baadhi ya njia hizo zinaweza kuwa ni kumuuliza moja kwa moja alikupendea nini, wewe kutumia muda kujifunza yeye anapenda nini kwako, kujifunza yeye anapenda nini kwa ujumla na uone kama inahusiana na wewe. Wakati mwingine unaweza kujua yeye anakupendea nini kwa kusikiliza na kuelewa ni vitu gani huwa hawapendei wengine. e.g. Unaweza kumsikia akisema maneno kama: "huwa sipendagi wasichana/wanawake wenye...", hapo unaweza kuelewa jambo...

Kwa bahati mbayai, kwa baadhi ya wanaume, huwa sio rahisi kupata majibu ya swali hilo kwa urahisi, kwa sababu zao nyingi ambazo hutofautiana – SIO WANAUME WOTE WATAKUAMBIA KIRAHISI TU NI KWA NINI ANAKUPENDA WEWE NA SI WENGINE!!!

Kuchumbiwa/Kuolewa Sio Mwisho

Sehemu na ya pili na ya muhimu sana kwako mwanamke, ni kuelewa namna utajitunza na kutunza kile alichokupendea mwenzako. Tambua kwamba, MNAPOKUBALIANA KUWA KATIKA UHUSIANO (uchumba au ndoa) SIO MWISHO WA MCHAKATO WA MAPENZI BALI NDIO MWANZO. Kwa hiyo ni lazima uelewe ni mambo yatakayoendeleza ari na hamasa ya mapenzi miongoni mwenu baada ya hapo. 

Kwa bahati mbaya, Wanawake wengi wanapoingia katika mahusiano, HUSUSAN AKISHAOLEWA huwa anaona kama vile ndio mwisho wa “mchakato wa mapenzi.” Matokeo yake wengi huwa hawajali tena wala kufuatilia ni kitu gani kilimfikisha katika uhusiano! Wengi hujiachia na kujiona ndio 'ameshafika', kumbe safari ndo imeanza!!

Ni lazima uelewe ukipendwa wewe sio kwamba ndio mwisho wa kupenda kwa huyo mwanamme wako, inaweza kuwa AMEAMUA kuacha kupenda tena (na kuishia kwako); LAKINI haimaanishi HANA UWEZO wa kupenda tena! Jifunze na uelewe ni namna gani uamuzi wake wa kupenda unaweza kuishia kwako, na asipate mawazo mengine tena ya kuendelea kupenda “kwingine” akiwa na wewe tayari!

Ni jambo la muhimu sana kuelewa kwamba huyo mwanamme hakukupenda kwa sababu tu wewe ni mwanadamu, amewaona na kuwaacha wanadamu wengi sana kabla yako lakini akakuchagua wewe. Hivyo ni muhimu sana uelewe kilichokutofautisha wewe na hao wengine ni nini, ili uelewe namna gani utaendelea kuwa tofauti na hao wengine siku zote!

Mifano

Kwa bahati nzuri/mbaya sababu za wanaume kuwapenda wanawake ndizo huwa ziko wazi zaidi kuliko kinyume chake. Kwa sababu hiyo tutaangazia baadhi ya sababu ambazo wanaume huzitumia kumchagua mwanamke wa kuishi naye, na namna gani mwanamke akikubali kupendwa anakuwa na wajibu kwa upande wa “kuzitunza” hizo sababu ili huyu mwanmme aendelee kuwa na sababu za kuendelea kumpenda huyu mwanamke.

Baadhi ya vigezo ambavyo wanaume huvitumia katika kuchagua mke ni Uzuri wa Sura, Tabia, Umbile la Mwili, Saizi ya Mwili (mnene/mwembamba), rangi ya ngozi, kimo, upeo wa ufahamu, elimu, dini, kabila n.k. n.k. (kumbuka si lengo la mkala hii kujadili uhalali wa hivi kuwa vigezo vya kumchagulia mtu, hilo huwa ni suala binafsi la mchaguaji). Hapa tutaangalia zaidi nafasi ya vigezo hivi katika kuendeleza uhusiano.

Wanawake wengi sana huwa hawapendi kuambiwa kuwa amependewa saizi ya mwili wake (unene/wembamba) kwa sababu wengi huwa na hofu siku zote kwamba kuna siku anaweza akakonda/akanenepa hivyo mapenzi yakapungua/yakaisha! Hata hivyo, hata kama una hofu, bado hiyo inaweza kuwa ni sababu ya yeyey kukupenda. Kwa mfano, kuna wanaume ambao hata siku moja huwa haoni uzuri wowote wa kumvutia kwa mwanamke mwembamba (kama ma-miss na ma-model) na wengine ni kinyume chake! yote haya ni mapendeleo ya watu binafsi.

Kutunza Kiini cha Mapenzi

Kwa mfano, ukibaini kwamba mume wako alikupenda kwa sababu ya saizi ya mwili wako, inaweza kuwa ni wembamba au unene, ni muhimu sana ukajitahidi kwa kadri ya uwezo wako kutunza umbo lile alilolipenda. Nimependa kuchagua huu mfano kwa sababu ndio huwa unaonekana kuwa mgumu zaidi kwa wanawake walio wengi na hivyo wengi huwa hawapendi kukubali hiki kuwa ni kigezo cha kupendwa!  Wengi husikika wakisema, "akinipendea wembamba je nikinenepa?" USIWE NA HOFU, jambo la muhimu sana hapa kuelewa ni ile jitihada uliyo nayo au utakayoionesha ya “kujitunza” hata kama matokeo yatakuwa tofauti.

Changamoto ya kutunza maumbo ya miili ni kubwa zaidi kwa wakina mama wa mijini ambao maisha wanayoishi (lifestyle) huwa yanahamasisha miili kunenepa, hata kwa vyakula vichache sana (tofauti na wale wa maeneo ya vijijini). Jitahidi kumuonesha mwenzako kwa maneno na vitendo kwamba unapenda ku-maintain umbo alilokupendea, hata kama matokeo yanakuwa tofauti. Unaweza ukaonesha hivyo kwa uchaguzi makini wa vyakula unavyokula, kutokula ovyo-ovyo na kila kitu kianchopita mbele yako, ufanyaji wa mazoezi n.k. Kitu cha muhimu hapa ni kuonesha kwamba unapenda kuwa vile anavyopenda, ila ni kitu kilicho nje ya uwezo.

Kinamama wengi kwa bahati mbaya ‘wakishapendwa’ hujibweteka kwa kuamini kuwa hataniacha, tayari ni wangu, nimefunga naye ndoa kanisani, nina cheti cha ndoa, tayari nina watoto naye, yeye ni kiongozi (e.g wa kanisa au serikali hivyo atakwepa aibu ya kushindwa ndoa yake) n.k. Na kwa bahati mbaya zaidi, ni wanaume wachache sana watakaokuja na kukwambia mke wangu jitunze “hivi-na-vile” ili niendelee kukupenda. Mumeo anatarajia ulishafundishwa hivyo siku nyingi, na mama yako, shangazi zako na kwenye kicheni-pati chako! Hii pia inachangiwa na tabia ya wanaume kutokupendela kuongelea maswala binafsi ya watu, ikiwa ni pamoja na ya kwao wenyewe au watu wao wa karibu!

Kama alikupenda kwa sababu ya Ukimya na Utaratibu wako, jitahidi sana baada ya kuingia katika mahusiano, hususan ndoa, usianze kuwa ‘mapepe’ ETI kwa sababu ‘tayari’ ameshakuweka ndani. Tunza ile amana aliyokupendea ili pendo lake kwako liendelee kudumu.

Kama alikupenda kwa sababu ya upeo wako wa ufahamu aliouona kwako, jitahidi hata utakapo ‘ingia ndani’ usibweteke tu na kuwa ‘mama wa nyumbani’. Endelea kujinoa na kujifua kwenye eneo lako la “strength” ili uendelee kuwa strong ndani yake pia.

Ni muhimu sana kufahamu kwamba wakati mwingine hauwezi kuwa na sifa zote za mwanamke ambaye mumeo anampenda, LAKINI unaweza ukazitunza na kuziboresha zile chache ulizo nazo ili kuhakikisha kuwa unaendelea kuwa ‘tofauti’ na wanawake wengine machoni pa mwenzi wako.

KUMBUKA SIKU ZOTE, kile alichokupendea zaidi mumeo ndicho kinachokutofautisha zaidi na wanawake wengine wote waliobaki, sio pete ya uchumba wala cheti cha ndoa kinachokutofautisha nao KIMAPENZI kwake. Cheti na pete vinaweza kukutofautisha nao kwake KISHERIA lakini mapenzi ni hisia, hayabadilishwi au kushikiliwa na cheti au pete…

Tunza vizuri amana aliyokupendea mwenzio, utaendelea kuwa juu siku zote moyoni mwake! Usijibweteke na kujiamini kwa sababu tayari ‘unaye’, kumbuka haujushika moyo wake! Kama hauamini, ukweli ni kwamba ANAWEZA ASIKUACHE (kwa sababu za kisheria au kijamii), LAKINI AKAISHI NA WEWE AKIWA HAKUPENDI TENA KAMA MWANZO…. Maumivu zaidi yatakuwa kwako...

KWA WANAUME TU: Kama ungependa hii makala mkeo/mchumba aisome hii makala usijali lakini HAUNA NAMNA YA KUMPA, nitumie email yake halafu nita-forwardia ii ujumbe kimtindo.... teh teh teh but am sirias... nibonyezee msbillegeya@hotmail.com au 0716 881 516

Ni mimi mwana-wenyu,
... ustaadhi mussa

7 comments: