Thursday, July 21, 2011

MAPENZI: Wanaume na “Window-Shopping”!

Maisha ya mahusiano ya kimapenzi katika ya wanaume na wanawake huwa yanahusisha mambo mengi sana, mazuri kwa mabaya, yenye kuleta furaha na kuleta huzuni, yeye kujenga na kuvunja moyo na labda mengine ambayo huweza kuwa linajitokeza zaidi ni yenye kuleta maudhi.

Moja ya mambo ambayo huumiza sana wapenzi, na kuleta maudhi sana katikanafsi, ni kuwa na mpenzi wako halafu ukaona au kubaini wakati fulani katika mahusiano yenu kwamba anakuwa interested na mtu mwingine tofauti na wewe.

Mara nyingi sana katika mahusiano ya kimapenzi, wanawake ndio huwa waathirika wakubwa wa matatizo na miendendo isiyo mizuri katika mahusiano. Hii inatokana na sababu nyingi, ambazo sio sehemu ya makala yangu ya leo. Leo, napenda nijadili tatizo moja ambalo huwaumiza wanawake katika mahusiano, nalo ni tatizo la Window-Shopping za waume/wapenzi wao wa kiume.

Katika muktadha huu, window-shopping ni ile tabia ya mwanamme kuwa na mke/mchumba wake lakini bado akaonekana kuwa interested kwa namna moja au nyingine na wasichana/wanawake wengine. Kitendo hiki mara nyingi sana huwaumiza wanawake kwa kuwa mwanamke huanza kuhisi kwamba labda hapendwi, labda ana upungufu, labda anazidiwa mvuto na wengine, labda anaelekea kuachwa, labda mwenziwe amebadilika, labda… labda….. labda…..

Pamoja na sura nyingi zinazoweza kuwa zimejificha katika tabia hii, ambazo baadhi yake zinaweza kuwa hizo zilizokwenye hizo ‘labda’ hapo juu, Napenda kuwasaida kukuelekeza katika upande mwingine wa tabia hiyo miongoni mwa wanaume, ambao unaweza kuwa hauna madhara, au kama unayo, basi yakawa ni madogo sana, iwapo utaelewa. Swali la msingi unalopaswa kujiuliza na kulijibu katika hali kama hiyo ni: ALIKUPENDEA NINI?

Ni muhimu kufahamu kwamba mwanamme anapoamua kumchagua binti kuwa mpenzi/mchumba/mke wake, kwa kawaida huangalia vigezo vingi sana, na akisha vijumlisha hutafuta wastani. Ule wastani atakaoupata ndio humpatia jibu – AKUCHUAGUE WEWE AU ATAFUTE MWINGINE! Hii huwa ni kanuni ya msingi sana kwa mwanamme yeyote aliye-serious na mahusiano. Wanaume ambao humchagua mtu kwa kuangalia sifa moja tu huwa wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kubadilisha mawazo wakati wowote kuliko wale wanaochagua kwa vigezo vilivyotafutwa kwa wastani.

Wastani wa tabia huweza, kwa mfano, kujumuisha vitu kama sura, tabia, umbo la mwili, kimo, dini, rangi ya ngozi, kabila/uraia, uongeaji/ukimya, ucheshi/u-seriousness n.k. n.k. n.k. Kweli ni kwamba katika hali ya kawaida, ni vigumu ukawa na sifa zote hizo, au basi ni vigumu kuwa na sifa zote anazozitaka huyo anayekutaka wewe.

Lakini kwa kutumia kanuni ya wastani, mwanamme anaweza akaridhika na wewe na akakutwaa wewe na kuwaacha wengine. Hii haimaanishi kwamba wewe ndiye unazo sifa zote anazozipenda mume wako kuliko wanawake wengine wote – HAPANA! Inawezekana kabisa wakawepo wanawake wenzio ambao wana baadhi ya sifa ambazo mumeo anazipenda na wanakuzidi hata wewe machoni pake, lakini wewe umewazidi kwa wastani na wingi wa sifa anazozitaka.

Kwa mfano, baada ya mumeo kutafuta wastani, alibaini kwamba japo hauna sura nzuri sana au umbo zuri la mwili, lakini una tabia nzuri sana kuwapita wale walio wazuri wa sura kukupita wewe, au wewe ni kabila ambalo yeye analipendelea zaidi, hivyo ukawapiku wale wengine ambao katika hayo maeneo mengine wanaweza kuwa wame-supp.

Utofauti huu unamaanisha kwamba, hata pale mumeo atakapokuona, haimaanishi kwamba wewe ndiwe mzuri kwa sura kuliko wanawake wote duniani, LA HASHA, ila tu ni kwamba wewe ndiwe unafaa kuwa mwenzi wake kwa sababu una sifa nyingi zaidi ambazo yeye anazihitaji maishani mwake kuliko wale wengine ambao wanaweza kuwa na sifa moja wamekuzidi sana lakini nyingine zote hawanazo – HIVYO AKAWAACHA NA KUKUCHAGUA WEWE!

Katika hali kama hiyo, mnapoendelea kuishi, mara moja moja unaweza kujikuta ukibaini kwamba mumeo hupenda kuwaangalia sana wanawake wengine, hususan wale ambao hata wewe unaweza kuona wana tofauti na wewe ambayo wewe hauna – kama uzuri wa sura au maumbile ya mwili – na ukabaini kwamba yawezekana mumeo anavutiwa zaidi na sura/maumbo yao kuliko la kwako. NI KWELI ANAWEZA KUWA ANAVUTIWA NAO LAKINI SIO KIGEZO PEKEE ANACHOKITUMIA KATIKA KUMCHAGUA ANAYEMFAA! Ukiwa na mume wa namna hiyo usiogope, atawaangalia hao wengine lakini mwishoni atakumbuka ni kwa nini alikuchagua wewe – NI KWA SABABU ULIWAZIDI HAO WENGINE WOTE!

Jambo la msingi unalopaswa kulielewa, kuliweka moyoni mwako na kulizingatia NI KUELEWA YEYE ALIKUPENDEA NINI! Ukishaelewa yale yaliyomfanya akavutiwa na wewe na kukuchagua, yashike sana hayo, shika kuyatunza, kuyaenzi na kuyaboresha kila iitwapo leo, ili kila siku aendelee kuamini kwamba hakukuchagua kimakosa.

Usifanye papara ya kutaka kujibadilisha ili ufanane na wale anaowaangalia sana na ukajikuta unayapoteza na kuacha kuyaboresha yale yaliyokupa alama za juu moyoni mwake hadi akakuchagua. Na kibaya zaidi ni kwamba katika kujaribu kujifananisha na wengine unaweza ukapoteza yale mazuri aliyokupendea na pia ukashindwa kuufikia uzuri wa wale unaotaka kujilinganisha nao – ukakosa mwana na maji ya moto.

Kuna mifano mingi sana ya wanawake ambao wamejiharibu sura na maumbo yao ya mwili kwa kutaka kujibadilisha ili wafanane na wale ambao anaona mumewe anawaangalia sana! Woman, Be yourself, onesha kwamba unajitambua na unajiheshimu kwa hivyo ulivyo, mwenzio atakupenda zaidi. Hauwezi kupendwa na kuthaminiwa iwapo utaonesha dalili zozote za kutokujitambua, kutojithamini, kutojiamini na kutojiheshimu kwa hivyo ulivyo.

BINAFSI NIMESHAKUTANA NA WANAWAKE WENGI AMBAO KWA KUMWANGALIA SURA TU HAUWEZI AMINI KAMA KUNA MWANAMUME ANAWEZA KUMUOA (hususan ukilinganisha na wale wanao-“zunguka” barabarani leo)! Lakini ukikaa naye karibu na kuchunguza mwenendo wake, unaweza kubaini ni kwa nini aliweza kuchaguliwa kuwa mwenza wa maisha wa mtu fulani!!!!!!!!!!!!!

hata hivyo, kuwa makini, asije akaangalia hadi akapitiliza huko huko... teh teh teh

Wasaalam,
Mwana wenu,
…mussa

No comments:

Post a Comment