Wednesday, May 9, 2012

Elewa Maana ya "Right Wing" na "Left Wing" katika Siasa


Moja katika ya maneno ambayo hutumika zaidi katika vyombo vya habari na siasa kwa ujumla katika dunia ya leo ni "Mlengo wa Kulia (Right Wing)" na "Mlengo wa Kushoto (Left Wing)". Leo nimeona ni vizuri kuangazia asili ya maneno hayo, matumizi yake ya mwanzo na maana yake halisi katika siasa za sasa.


Mnamo mwaka 1789, baada ya Vuguvugu la mapinduzi nchini Ufaransa, kwa mara ya kwanza liliundwa bunge la kitaifa ambalo lilikuwa na pande kuu mbili - Upande Mmoja ni wale Waliotaka Mabadiliko, Mamlaka na uhuru zaidi kwa wanachi - yaani kupunguza mamlaka ya Mfalme juu ya masuala ya Utawala wa Nchi na kuyapeleka zaidi kwa Wananchi. Na upande wa pili ulikuwa ni wale waliokuwa upande wa Mfalme - waliokuwa wanatetea na kulinda maslahi ya Mfalme na tabaka tawala katika Ufaransa ya wakati huo!
Mikao Bungeni haitegemei Upande Ki-Aidiolojia bali kiutawala
Bungeni, makundi haya mawili yalikuwa yanakaa pande mbili tofauti (walikuwa hawachanganyikani). Waliokuwa wanataka Mabadiliko (wapingaji wa tabaka tawala) waliketi upande wa Kushoto wa Spika na waliokuwa hawataki mbadiliko, (Mahafidhina), walikuwa wanaketi upande wa kulia wa Spika - Utaratibu huu unaendelea mpaka leo katika mabunge yote duniani - Hadi Dodoma, Tanzania!

Kwa hiyo, wale waliokuwa wanatetea na kulinda tabaka Tawala waliitwa Mlengo wa Kulia (Right Wing, Conservatives) na wale waliokuwa wanataka mabadiliko waliitwa wa Mlengo wa Kushoto (Leftists / Left Wing, Liberals).

Hata hivyo, katika matumizi ya kawaida SIKU HIZI, Left Wing na Right Wing huwa sio istilahi zinazohusu zaidi nani anatetea Tabaka tawala na nani analipinga, bali zaidi Ni nani anatetea Maslahi ya Taifa/Utaifa zaidi na nani anataka Uhuru na Mabadiliko zaidi - hususan wanaotaka Muunganiko na Muingiliano zaidi wa Jamii na Mataifa mbalimbali na wageni!... Ndio maana katika nchi zilizoendelea, moja ya hoja za msingi ambaz hutofautisha milengo ya vyama na watu ni suala la uhamiaji - wenye mlengo wa kulia hupinga kabisa masuala ya kuruhusu wahamiaji kutoka nje kuingia - na hususan kupewa haki kama raia wazawa, wakati wa mlengo wa kushoto huwa wazi na suala zima la wa hamiaji - wote kwa sababu tofauti.

Kwa hiyo,katika siasa za sasa, suala la kuwa mlengo wa kushoto au wa kulia halifungamani sana na kuwa madarakani au kuwa upinzani - bali linahusu zaidi aidiolojia ambayo mtu husika au chama inaisimamia. Kwa maana hiyo, Kuwa madarakani au kwenye Tabaka tawala hakumfanyi mtu akawa ni Right wing, anaweza akawa madarakani huku akiwa ni mlengo wa Kushoto (Liberal) ki-aidiolojia, na bungeni ataketi Mkono wa Kulia wa Spika, lakini akiwa ni Left wing Kisiasa / kiaidiolojia! Jambo la Msingi katika kutambua Mlengo wa Siasa katika dunia ya sasa huwa ni msimamo wa mtu kuhusu Taifa na Utaifa. 
Tofauti za Kiaidiolojia ndizo husema nani wa "Kushoto" au "Kulia"

Wanaoweka taifa na utaifa wao mbele ndio huitwa Mahafidhina, Mlengo wa Kulia, na wale wanaoweka mbele "uhuru zaidi" kama kukaribisha na kutetea uwekezaji wa nje, mafungamano ya kimataifa n.k. huitwa Mlengo wa Kushoto.

Kwa mfano, marekani kwa sasa inatawalia na Mwanasiasa wa Mlengo wa Kushoto / Left wing / Liberal (Obama / Democrats). Hiki ni chama kinachoamini katika uhuru zaidi wa watu, kiko wazi zaidi katika muingiliano na ushirikiano na mataifa na watu wa mataifa mbalimbali zaidi na wageni kuliko chama cha upinzani ambacho ndicho cha kihafidhina - Republican! Rais aliyeshinda Ufaransa wiki hii ni wa Mlengo wa Kushoto-Kati (F. Hollande / Center-Left) kwa kumshinda Mhafidhina-kati (Center-Right) Sarkozy.

Kwa maana hiyo tunaongeza dhana nyingine hapo ya muhimu kuielewa, Center-Right na Center-Left. Hizi ni pande ambazo haziko ki-viile katika hiyo milengo, tunaweza kusema ni milengo  yenye aina fulani ya Uvuguvugu, ambapo husimamia masuala makuu ya upande wake (Kulia au Kushoto), wakati huo ikikubaliana na baadhi ya yale yaliyo upande mwingine...

tujadili pamoja, Je, wewe unadhani kwa Tanzania, ni vyama gani viko mlengo wa kulia na vipi viko mlengo wa kushoto? weka maoni yako hapo chini kwenye comments!

5 comments:

  1. Mi nadhani kwa chama kilichoko madarakani, hakifuati mlengo wowote ule. Kila mtu analinda tumbo lake na la yule aliyemuweka. Sidhani kama wanasiasa wengi wa kwetu wanajali sana watu wake au utaifa wake...

    ReplyDelete
  2. Ccm inafuata mlengo wa center-light wingi

    ReplyDelete
  3. hapana,nadhani haifungamani na upande wowote hila tu utegemea na vipaumbele vya mwenyekiti wa chama(raisi wa jamuhuri),utaifa kwanza au masuala ya mahusiono na jamii za kimataifa, kwahiyo muda mwingine siasa kati za mlengo wa kushoto na mda mwingine siasa kati za mlengo wa kulia.

    ReplyDelete