Monday, January 16, 2012

MAREHEMU REGIA MTEMA: Wasifu, PICHA na Maelezo ya Ajali

Marehemu Regia Mtema
Wasifu wake Kwa Ufupi
Marehemu Regia Mtema alizaliwa Aprili 21, 1980. Alisoma elimu ya msingi kati ya mwaka 1989 na 1995. Alijiunga na Shule ya Sekondari Forodhani, Dar es Salaam mwaka 1996 hadi  1999 na kuhitimu kidato cha nne.  Aliendelea kidato cha tano 2002 na sita kati ya mwaka 2000 na 2002 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Machame, mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari


Mwaka 2003 hadi 2006 alisoma Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na kupata Shahada ya Maarifa ya nyumbani na Lishe. Baada ya kuhitimu shahada yake, marehemu Mtema alifanya kazi katika taasisi mbalimbali kabla ya kujiunga na Chadema na kuteuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Vijana ya chama hicho.
Mwaka 2010 aligombea Ubunge katika Jimbo la Kilombero


Baadaye aliteuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Mafunzo ya chama hicho, nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka 2010 alipoteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum.

Marehemu enzi za uhai wake akiwa
katika Viwanja vya Bunge Dodoma




Maelezo ya Ajali

Muonekano wa Mbele wa Gari alilokuwa akiliendesha Marehemu
Marehemu Regia alikuwa anaendesha gari aina ya Land Cruiser VX Limited (V8) lenye namba za Usajili T296 BSM. Ajali hiyo ilitokea mnamo saa 5:30 asubuhi katika maeneo ya karibu na Sekondari ya Ruvu. Ajali ilitokea pale Regia alipotaka kulipita gari lingine lililokuwa mbele yake na ghafla aliona gari jingine likija mbele yake kwa kasi.
Muonekano wa Pembeni

Ili kuepusha kugongana na lile gari lingine uso kwa uso alikwepesha gari lake na ndipo liliacha njia na kupinduka. Watu wengine saba waliokuwa naye kwenye gari hilo walilokuwa wakisafiria kuelekea Morogoro walijeruhiwa tu.
...
*************************************************************************
R.I.P REGIA ESTELATUS MTEMA


4 comments:

  1. Tumempoteza mpiganaji hodari. RIP Regia Mtema

    ReplyDelete
  2. R.I.P REGIA BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE.

    ReplyDelete
  3. Mungu Amlaze mahali pema peponi jamani dada Regia, pengo lake haliwezi kuzibika kamwe! R.I.P sister

    ReplyDelete
  4. mungu amlaze mahali pema peponi.Amen

    ReplyDelete