Wednesday, May 30, 2012

UDINI: TAMKO la WAISLAMU Dhidi ya WAKRISTO!

 Utangulizi
Oktoba 31, 2010 Tanzania ilifanya uchaguzi mkuu ambapo wananchi walipata fursa ya kumchagua Rais, wabunge pamoja na madiwani. Katika uchaguzi huo, Watanzania kwa ujumla wao walikichagua Chama cha Mapinduzi, CCM, kuongoza tena nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Hata hivyo, wakati wananchi wakiamini kwamba wanaongozwa na watu waliowapigia kura, matukio yanayoendelea hivi sasa yanaashiria serikali kutelekeza majukumu yake na kuwaacha maaskofu wakielekeza nchi wanakotaka.

Itakumbukwa kwamba awali kabla ya uchaguzi mkuu maaskofu walikuwa wametoa Ilani yao ya uchaguzi bila kueleza kipi chama chao kitakachosimamia na kutekeleza Ilani hiyo. Baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala, CCM, walishabikia Ilani hiyo na kuwatetea maaskofu. Kwa hakika taarifa za vyombo vya habari zilifahamisha kwamba baadhi ya watendaji waandamizi ndani ya serikali walishiriki katika kuandaa Ilani hiyo.

Ilipofika wakati wa kampeni hadi kuingia siku ya kupiga kura, ilikuwa imedhihiri kipi kilikuwa chama cha maaskofu ambacho walitarajia kitekeleze Ilani yao. Haikuwa tena jambo la siri kwani walisimama wazi wazi kuwaelekeza waumini wao wampigie nani kura. Na katika juhudi zao za kutaka wafuasi wao wawaelewe vizuri, maaskofu walithubutu hata kuweka kando mafundisho ya Biblia yao juu ya masuala ya uzinzi wakawahimiza waumini kumpigia kura mtu wanayemtaka bila kujali kwamba anakabiliwa na kashfa ya kupora mke wa mtu. Waliwaambia wasihangaike na maisha binafsi ya ndoa ya mgombea.
 
Hata hivyo, matokeo ya kura yalitoa majibu kwamba Watanzania walikuwa wameikataa Ilani ya Maaskofu.

Waislamu tumelazimika kukutana na kutoa tamko hili kwa sababu matukio yanayotokea hivi sasa yanaonesha kuwa wale ambao Watanzania walikataa kuwapa uongozi na Ilani yao iliyoandaliwa na maaskofu, ndio sasa wanaielekeza nchi pa kwenda huku viongozi wa CCM na serikali wakijitahidi kadiri ya uwezo wao kunyenyekea kwa maaskofu hao.

Tumeona na tumemsikia Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda akihangaika kuwapigia magoti na kuwaomba radhi maaskofu kule Sumbawanga. Tumesikia jinsi viongozi wanaojaribu kuwaambia maaskofu kwamba kama wanataka kuingia katika siasa wavue majoho na vyeo vyao vya kikanisa kama Padiri mwenzao waliyekuwa wakimpigania kuingia Ikulu, wanavyokemewa na kutakiwa wawaombe radhi maaskofu hao.
 

Lililo baya zaidi maaskofu walioshindwa kuwashawishi wananchi waipokee na kukubali Ilani yao, wamekuja na kampeni za kuchochea uasi kwa serikali iliyopo madarakani. Lakini pamoja na hali hiyo, viongozi wa CCM na serikali wamebaki wanagwaya. Hakuna aliyeweza kupata ujasiri wa kukemea hali hii. Kinyume chake Waziri Mkuu na Mzee John Samwel Malecela wanahangaika huku na kule wakiwapigia magoti maaskofu hao na kuwakemea wanaothubutu kuwakosoa.

Hali kama hii ni hatari kwa usalama na utulivu wa nchi. Ni hali ya kuchochea udini na kuweka ombwe la uongozi wa kisiasa ambao utazua balaa. Waislamu hatuwezi kukubali hali hii. Kwa hiyo, ama CCM na serikali vitekeleze wajibu wao wa kuongoza au kama wanaona hawawezi, basi waseme rasmi ili Maaskofu na wengine wenye Ilani zao za uchaguzi waingie tena ulingoni kuomba ridhaa ya Watanzania kuongoza nchi kuliko kuishi katika hiki kiini macho ambapo maaskofu na mawakala wao ndani ya serikali wameachwa waikokote nchi wanakotaka.
 

Kiini cha Hali hii ya Kisiasa
Hali hii ya kisiasa tunayoishuhudia leo nchini mwetu ni matunda ya mbegu liliyopandwa na kupaliliwa kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita. Wakoloni walikuwa na kanuni yao waliyoiita divide et impero yaani wagawe ili uwatawale. Huko Rwanda wakoloni waliwagawa wananchi kwa misingi ya kikabila. Watusi ambao ni watawala wapewe elimu ya juu na wanfundishwe kwa Kifaransa, na Wahutu ambao ni watawaliwa wapewe elimu duni na wafundishwe kwa Kiswahili. Ubaguzi huo wa kuwagawa raia wa nchi moja ulipandikiza sumu iliyokuja kusababisha Wanyarwanda kuuana.

Hapa kwetu wakoloni walitugawa kwa misingi ya dini. Kabla ya uhuru wa Tanganyika, wakoloni kwa kushirikiana na makanisa waliwaona Waislamu kama ni mahasimu wao kidini na kisiasa. Na kwa sababu hiyo serikali za kikoloni zikaweka mikakati maalum ya kuwakandamiza Waislamu katika maeneo matatu: kwanza kuwawekea vikwazo katika kutangaza dini yao ili wasiongezeke; pili kuwabana katika elimu na ili kuhakikisha kuwa Waislamu wanabanwa jukumu la kuwaelimisha Waafrika likawekwa mikononi mwa makanisa na kazi ya serikali ni kuzigharimia tu shule hizo. Lengo likiwa ni kuwabatiza Waislamu wachache watakaoruhusiwa kusoma, na tatu kuwabana katika ajira serikalini kwa sababu makanisa yote yalisisitiza kuwa kuwaajiri Waislamu serikalini ni kusaidia kuenea kwa Uislamu..
 

Kwa kuwa ubaguzi huo haukuwa na kificho chochote, Waislamu wengi walijitokeza kupambana na ukoloni kwa matarajio kuwa serikali huru itaondosha chuki na uadui huo dhidi ya Waislamu. Lakini msiba mkuu wa taifa hili ni kwamba kinyume chake, baada ya uhuru msimamo ukawa ni ule ule wa kuwaona Waislamu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na mikakati ya kuwabana Waislamu katika maeneo yale matatu ikaimarishwa zaidi wakati wa utawala wa Nyerere. Kuanzia 1957 mkakati uliopangwa na Kanisa Katoliki ukawa ni kuhakikisha kuwa nafasi zote muhimu za uongozi na serikali zinashikwa na wao. [Taz. Confidential Diary – Tanganyika, March-April 1957, uk. 3-4 Maryknoll Central Archives, New York ]. 

Na ni mkakati huu ndio ambao Mwalimu Nyerere aliokuwa akimuhakikishia Askofu Rweyemamu mwaka 1970 kuwa anatumia mamlaka yake kama Rais na kama kiongozi wa TANU kuhakikisha kuwa anatoa upendeleo maalum kwa Wakristo ili wasimamie sera za Chama. Na kwamba amemteua padiri katika nafasi nyeti ya Chama si kwa sababu anajua siasa bali kwa sababu ni Mkristo safi. Lakini Nyerere huyo huyo akisimama hadharani alijidai kukemea udini. Na kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuliimarisha kanisa na kuwadhoofisha Waislamu, leo Kanisa lake limo katika mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa ni Mtakatifu!
 
Sivalon anaarifu katika kitabu chake kuwa mara baada ya uhuru Kanisa katoliki liliwahamasisha Wakristo wote na hasa watendaji wa serikali juu ya hatari ya Ukomunisti na Uislamu na walikusanya nguvu zao zote katika kukabiliana na maadui hao.

Matokeo ya Hujuma Hizo
Matokeo ya hujuma hizo za kichinichini ni kwamba katika sura ya nje na katika propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na kisiwa cha amani. Lakini uhalisia wa mambo ni kuwa Tanzania ni nchi yenye jamii kubwa mbili. Jamii ya Wakristo wanaopewa msaada, upendeleo, ulinzi na heshima, na jamii ya Waislamu ambao wanachukiwa, kudharauliwa na kudhoofishwa na serikali kabla na baada ya Uhuru.



Maazimio ya Waislamu
Kwa kuzingatia muktadha wa hali ya kisiasa ilipofikia hivi sasa, Waislamu tumefikia maamuzi yafuatayo:

(1) Maadam Mfumo Kristo umeimarika kiasi cha kuweza kuitisha serikali na viongozi wake na wakatishika, na maadam Mfumo huo Kristo una nguvu za kuweza hata kuvitisha na kuvikemea vyombo vya dola na vikasalimu amri, Waislamu tutake tusitake, kama alivyohadharisha Mh. Membe, ukweli unabaki kuwa hautapita muda mrefu, dhulma hii ya udini italisambaratisha Taifa letu, kama udini ulivyoisambaratisha Ivory Coast ambayo katika miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa mfano wa kuigwa.

Hivyo basi wajibu wetu wa mwanzo ni kuufikisha ujumbe huu kwa Waislamu wote nchini, na kuwataka wazingatie kuwa kwa kuwa wanabaguliwa na kudhalilishwa katika nchi hii kwa sababu ya Uislamu wao, basi ni wajibu wao na wao kushikamana kama Waislamu.
 

(2) Kwa kuwa kila wanchosema Maaskofu ndicho kinachofuatwa na serikali, na kwa kuwa Maaskofu wamekwishatamka hadharani na kwa sauti kali kuwa katika nchi yetu hakuna kabisa udini na atakayesema kuna udini basi ni yeye ndiye anayetaka kuleta udini, na kauli hiyo kudakwa na mawakala wa Maaskofu katika serikali, ni dhahiri kuwa dhulma za udini zinazoendelea kuwakandamiza Waislamu miaka 50 baada ya Uhuru hazitaondoshwa na Katiba mpya. Hivyo wajibu wetu mwingine ni kupigania ukombozi wa Waislamu ili washiriki katika kuandaa katiba mpya wakiwa ni raia huru na sawa na wenzao. Waislamu popote tulipo tunao wajibu wa kuorodhesha dhulma zote za udini tunazofanyiwa na kupigania ziondolewe kwanza na kulipwa fidia.

(3) Kwa kuwa tangu ukoloni hadi leo Waislamu wanahesabiwa na serikali na Maaskofu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na wasiostahiki haki sawa na wengine, na kwa kuwa Waislamu wameazimia kutokukubali tena kudhulumiwa na kuonewa kwa namna yoyote ile iwayo, ni wazi kuwa hakuwezi kuwa na katiba itakayoweza kulinda haki za madhalimu na wadhulumiwa kwa wakati mmoja. Ingawa kwa propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja, lakini kiuhalisia ni nchi yenye jamii mbili zenye hadhi na haki tofauti kabisa. 


Umefika sasa wakati wa kugawana nchi ili Waislamu wanaochukiwa na kunyimwa fursa sawa na Wakristo waishi katika maeneo yenye Waislamu wengi na Wakristo waishi katika maeneo yenye Wakristo wengi. 

Mwalimu Nyerere alipigania kwa nguvu zake zote Nigeria igawanywe ili Wakatoliki ambao walikuwa wanadhulumiwa Nigeria wajitenge na waruhusiwe kuishi katika nchi ya Biafra. Na katika kijitabu alichokiandika 1966 Nyerere alisema madai ya kuhifadhi umoja wa kitaifa wa Nigeria hayana maana yoyote pale ambapo baadhi ya raia wa taifa hilo wanadhulumiwa. Ushahidi wa dhulma za Waislamu upo wazi. Kugawana nchi kutawawezesha Waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC bila ya kuwakera Maaskofu. Ni wajibu wetu kulifikisha hili kwa Waislamu wenzetu nchi nzima ili lijadiliwe zaidi kabla halijafikishwa rasmi

(4) Kwa kuwa hakuwezi kuwa na amani ya kweli bila ya haki, na kwa kuwa amani ya Tanzania inashikiliwa na Waislamu walioruhusu dhulma hiyo, Waislamu tunayo dhima kubwa kwa kustawi kwa Mfumo Kristo ambao sasa hapana shaka yoyote unalisambaratisha Taifa. Lakini kama alivyosema Nyerere, anayedhulumiwa ni mtu anayeteseka. Asipopambana na huyo dhalimu, yeye ataendelea kuteseka wakati dhalimu anastarehe kwa amani. Akiamua kupambana, wote yeye na dhalimu watateseka.  


Baada ya miaka 50 ya kuachia kundi moja la jamii likistarehe na hali Waislamu wanateseka, umefika wakati sasa wa kugawana machungu ya udini tuliyoyabeba peke yetu kwa miaka hamsini.

20 comments:

  1. MBONA WANALIALIA SANA HAWA JAMAA,MIMI SIONI JITIHADA ZA KUJINASUA HAPO WALIPO ZAIDI YA KUMLAUMU NYERERE,HAYA MWINYI ALIFANYA NINI,NA SAIZI MNAYE KIKWETE HAKUNA KITU HAPO.

    ReplyDelete
  2. tumieni akili nyie mnaofanya kampeni hizi za kishamba na kijinga. Mtu mzima unadiriki kuongea upuuzi ili tu kuanzisha vita kwenye nchi yetu?.embu tuambie umepanga kufaidika nini na hiyo vita?..maana ni lazima una faida unaisubiria na sio kweli kwamba unapigania uislamu.ulaaniwe wewe na kizazi chako. Mwenyezi Mungu ashushe radi yenye laana na magonjwa na mabaya yote kwako wewe na uzao wako wote wewe unayefanya kampeni hii inayolenga kutuletea matatizo yasiyo na msingi katika nchi yetu. Unakaa na kuiga upuuzi unaotokea kwenye nchi nyingine na kutaka kuuleta kwetu Tanzania. kwanini usiige mambo ya Kimaendeleo?. Kama kwako kumwaga damu ndiyo akili basi mwaga damu za ndugu zako na utuachie nchi yetu ikiwa salama na ya amani. Hakuna sehemu ya Msaafu inayosema muislamu safi ni yule anayechochea vurugu za umwagaji damu. jifunze kuwa na busara na akili badala ya kukurupuka na kusambaza ujumbe wa kitoto usio na msingi wowote. Tanzania ina shule nyingi sana, na inaonesha unahitaji kurudi shule usome na kupanua ubongo wako. Uislam ni amani,upendo na mshikamano na sio vita na uchochezi.

    ReplyDelete
  3. BLOG ZAKISHENZI KAMA HIZI NINGEKUWA GOOGLE NINGESHA ZIFUNGA....WAISLAMU NIWAPUMBAVU SANA NA WACHOCHEZI>>>>UMASIKINI NA UKOSEFU WA ELIMU NDO UNASUMBUA....NAWAAMBIENI HATA MSEMAJE ANZISHEN VITA VYA KIDINI MUONE..KUMBUKA WAKRISTO TUKO ZAIDI YA 60% NA NYIE NI 30% TU KWA IDADI YA BARA NA VISIWANI...USIDHAN UKIMYA WA WAKRISTO NDO MWANYA WA UCHOKOZ WENU

    ReplyDelete
    Replies
    1. nadhani kuwa mshenzi utakuwa wewe kwa kuwajumuisha waislam ktk matamshi yako, kumbuka kila mtu awe muislamm ama mkristu ana upeo tofauti ktk kuchambua mazungumzo, nadhani elemu yako ipo ktk ukosefu wa hekima na busara, uwingi wa 60%, na uchache wa 3o% bado ni wazo la kipumbavu kama huyo mwenye hii blog, mmhkumu mkosaji peke yake usijumuishe wote, usiwe na akili mgando, na iliyojaa matope, na bora ya umasikini wa waislam kuliko wewe uliye masikini wa akili na mwenye elimu ya kijinga, na ya kipumbavu, hujui hata unachangia nini humu, koma kama ulivyokoma ziwa la mamiyo, kuwatukana waislam

      Delete
  4. Ndugu Wachangiaji, Tamko hili lililowekwa hapo juu ni Tamko lilitolea na Jumuiya Waislamu Tanzania Mwezi Januri mwaka 2011 na Kuchapisha katika Vyombo Vingi vya habari (NA SIO Tamko la BLOG Hii)!

    Hakika Serikali na Vyombo vingine husika vilipaswa kuchukua Hatua Kukemea Waliotoa Tamko hilo lenye Uchochezi, na Kujiandaa kuzuia Vitendo viovu ambavyo vingefuata kutekeleza Tamko Hilo (kama inavyotokea Zanzibar)! - ASANTENI!

    ReplyDelete
    Replies
    1. sio kukemea tu bali na kuangalia na kuchunguza kama madai hayo ni sawa basi na wapewe, ambayo ni haki na sawa kwa wote, na kama ni ya uongo wachukuliwe hatua za kisheria na wahukumiwe kulingana na makosa yao, kwani ni hatari sana kunyamazia matamshi makali kama haya ambayo yanaweza kusababisha mauaji makubwa ktk nchi, mfano kwa haya tu yaliyotufikia baadhi ya wachangiaji wameweza hata kuwaita waislam ni washenzi na wenye elimu dhaifu, kiasi ambacho haya yakiendelea ktk kuwajumuisha waislam wote huoni kuwa yataanza kuzua yasiyo muhimu kwa jamii ya watu waliostaarabika?

      Delete
  5. Na wewe uliyebandika hapa utueleze ulikuwa na lengo gani. Kama wewe ungekuwa na akili usingesambaza matamshi ya kichochezi na ya kipuuzi hapa ukitegemea watu waifurahie kazi yako!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hili ni tamko ambalo lilitolewa Wazi wazi na kuchapishwa na vyombo vingi vya habari, redio na televisheni. Lengo la kuweka hapa ni ili Watanzania wengi zaidi wasome na kuelewa kwamba Tanzania kuna kundi la namna hii ambalo linahubiri na kueneza uchochezi hivyo Watanzania wote kwa pamoja Wajadili na Kuchukua hatua za pamoja...

      Kutokujua uwepo wa Tatizo haimaanishi mtu hataathirika na tatizo husika, maarifa ndio ufunguo, tuelewe na tuchukue hatua!

      Delete
  6. Pumbavu zenu rudini shule mkasome. Mnabaki kujadili tu dini za wenzunu in amaana hamjiamini na dini yenu. Anzisheni hiyo vita basi muone au mnadhani watu kua kimya ndio watawagwaya. Mmezoea kula urojo tu na kufunga misuli

    ReplyDelete
    Replies
    1. mpumbavu ww usitukane uislam na waisalm tafadhali

      Delete
    2. hahahahahaaaaa......hii inafurahisha sana....

      Delete
  7. Matusi na Jazba havisaidii kubainisha Tatizo na Kulimaliza. Kama taifa, tukiongozwa na Serikali yetu, Kwa wakati huu tuna wajibu wa Kufanya taathimini ya kina ya Malalamiko na Matatizo yaliyopo na kuyapatia Ufumbuzi - kwa manufaa ya Watu wote!

    ReplyDelete
  8. uspoziba ufa utajenga ukuta,waliyosema ndiyo sasa yanatimia.ukicheka na nyani utavuna mabuwa.

    ReplyDelete