Marekani rafiki "mkubwa" wa Tanzania na Israeli |
Alipokuwa akihojiwa na Mtangazaji Ayala Hasson wa Kituo cha redio cha Israeli, waziri wa Ulinzi wa Israeli Ehud Barak alitoa maelezo ambayo kimsingi yalimaanisha Tanzania ni "Irelevant" kwa Israel. “Germany, France and England are not Tanzania, Mauritania or Tripolitania [jimbo mojawapo nchini Libya],”.... alieleza Ehud na kuongezea “These are very important, very relevant countries and we don’t have an interest in increasing tensions with them or making them bitter enemies.”
Reaction ya Tanzania
"Balozi wa heshima" wa Tanzania nchini Israel, Kasbian Nuriel Chirich alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli kulaani kauli hiyo ya Barak na kumualika kiongozi huyo kuitembelea Tanzania. Katika barua hiyo, "balozi" huyo pia alilaani kitendo cha Waziri Barak kuishusha hadhi Tanzania na kuilinganisha na nchi ambayo, kimsingi haipo hapa duniani (Tripolitania) ambalo ni jimbo tu nchini Libya!
Ehud Barak, Waziri wa Ulinzi wa Israel aliyesema Tanzania ni "Irrelevant" kwa Israel |
Ukweli wa Hali halisi!
Watu wengi wamejitokeza hapa Tanzania kulaani hiyo kauli ya Barak na kumtaka aifute na kuomba msamaha. Labda wako sahihi, lakini mimi napinga! Na sababu kubwa ya mimi kupinga NI UZALENDO WANGU!Maneno ya Barak ni ya kweli kwa kiasi kikubwa sana - "Tanzania is Irrelevant to Israel" na hata kwa mataifa mengi sana pia duniani! Mimi ninaamini kuna mataifa mengi mno duniani - hata wale wanaotupatia misaada ambao nao wanaiona Tanzania iko irrelevant kwao! Tofauti tu ni kwamba hao wengine ni wanafiki wakubwa hivyo wanapokuwa na viongozi wetu hujitahidi kuwaonesha kwamba wanawathamini kama watu na kama viongozi wa "taifa" fulani - ambalo ni irrelevant kwao - though!
Unapokuwa na taifa lenye rasilimali na utajiri mkubwa sana kama Tanzania lakini viongozi wake wanazurura duniani kote kuomba-omba misaada na wala hawana sauti katika masuala ya msingi ya kidunia - na hata yale ya nchi zao wenyewe - hizo nchi ni irrelevant kwa taifa kama Israel!
Mataifa mengi ambayo yana nguvu na ushawishi mkubwa hapa duniani - ikiwa ni pamoja na kwa Israel - ni yale ambayo, kwa kutumia rasilimali na utajiri wao wa asili na wa kutafuta, yameweza kuwa na nguvu na sauti kubwa duniani kiasi cha kuweza kuheshimiwa na Israel. Mataifa kama hayo aliyoyataja Ehud na mengine kama Urusi, Iran n.k. yemtumia vizuri utajiri wao na rasilimali zao kujiweka kwenye ramani ya "relevance" duniani kiasi kwamba Israeli inaelewa haina namna zaidi ya kuwa na mahusiano mazuri na nchi hizo.
Ehud anafahamu kabisa kuwa na urafiki au mahusiano mazuri na nchi kama Tanzania ni kujivutia omba-omba asiye na faida karibu yako. Niambie iwapo mahusiano kati ya Tanzania na Israeli yataimarika, ni nini zaidi Tanzania itakachokitafuta katika mahusiano ZAIDI YA KUOMBA-OMBA MISAADA kila iitwapo leo???
Huu ni ukweli ambao naamini hata Marekani wanaufahamu, ila uzuri tu ni kwamba wao ni WANAFIKI SANA kuliko Israel, hivyo wanaweza ku-pretend kutuheshimu wakati behind the curtain wanatuona kuwa tuko "irrelevant" kama Israeli tu wanavyotuona.
Ukweli ni kwamba kwa hali ya sasa ya Tanzania, hususan kwa uongozi na sera tulizo nazo na tunazotumia, TANZANIA IS IRRELEVANT kwa namna nyingi sana kwenye ramani ya dunia!
Masuala makubwa yanayoikabili Israeli kwa sasa ni pamoja na Nyuklia za Iran, Mapinduzi nchi za Kiarabu, Migogoro ya ndani ya Kiuchumi, Suluhu na Wapalestina n.k. Katika haya masuala yote, Tanzania haina nafasi yoyote relevant ya kuifaa Israel, hivyo tusimlaumu Ehud kwa lolote - yuko sahihi kabisa.
Hili linapaswa tu kuwa changamoto kwetu kama taifa, ni kwa muda gani tutaendelea kufanya mambo ya kulidhraulisha na kulitukanisha taifa letu kama kuwa na viongozi maomba-omba wanaozunguka dunia nzima kuomba misaada huku wamegawa utajiri wa taifa na rasilimali zake "bure' kwa wazungu?
Tunayo kazi ya kuifanya Tanzania Relevant! I SUPPORT ISRAEL!
My Bro Musa,
ReplyDeleteNakubaliana kwa sehemu kubwa ya ulichosema kuhusu umuhimu wa Tanzania kwa Israeli. NI ukweli ulio wazi kwamba ukilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, UK and German, sisi mchango wetu kiuchumi kwa Israel ni mdogo sana na huenda ikawa hakuna kabisa (sina data).
Pamoja na hayo, nadhani tunachepuka kidogo kutoka kwenye msingi wa alichodai mwakilishi wa Tz huko Israeli (hatuna ubalozi kamili huko). Alichodai balozi huyo ni kwamba usemi wa ehud umeonyesha DHARAU kwa nchi ya Tanzania kwa kuilinganisha na ka-jimbo huko Libya! Inawezekana kabisa ni kweli nchi yetu maskini... lakini point hapa ni kukosekana kwa uungwana wa kibinadamu kabisa kwa alichokisema ehud.
Kiubinadamu - jambo ambalo katika level ya nchi wangesema "kidplomasia"; JUST because mmoja wetu ana mali zaidi (how they got it is immaterial) AU ana sauti zaidi (how he/she got that voice is immaterial) katika mikutano ya jumuia; haiimpi haki kwa yeyote kumdharau yule ambaye hanacho (HATA kama hana kwa uzembe wake)! It is a simple human relations issue and diplomacy 101!
A few minutes kabla sijasoma entryyako, Nime "mblast" ehud kwenye blog yangu (http://my-bongo.blogspot.com) for simple reason... ameonyesha udhaifu mkubwa na wakizembe sana katika nyanja za kidiplomasia! Usemi wa ehud ume amount to tusi to a sovereign state! - ikiwa ni pamoja na sote tulio raia wa nchi hiyo! I sincerely do not care of the motive behind his remarks!... kutumia matusi au kumtusi mtu (BILA ya kuchokozwa kwa namna yoyote ile) demonstrate one motive and one motive ONLY - to dehumanize yule unayemtusi! INFACT: utumiaji wa matusi unaonyesha how primitive mtumiaji wa tusi alivyo! Katika hilo HAKUNA namna muungwana unaweza kuli justify!
NOW having said that: mwenye akili ni lazima kujiuliza iwapo kuna lolote ulilofanya kupelekea au kusababisha mtu wa pembeni kuonana (na kudhubutu kumtamkia kwamba you are) irrelevant! Nakubaliana kabisa na ukweli kuwa Katika hilo, tuna maswali mengi ya kujiuliza - na iwpao busara zitatumika kujaribu kurekebisha mazingira ili kujijengea uzio utakaosaidia kuzuia wengine pia kutuita "Irrelevant".
NIPO tayari kabisa kuwa na mjadala katika hili - ili kujiweka katika mazingira mazuri zaidi.
LAKINI katika usemi huu wa haka kajamaa - ehud, ni lazima nipinge vikali kabisa. Ukisoma ka entry kangu - utaona hata upendwa hakuna; NI maoni yangu kuwa; kama mwanadamu yeyote wa kawaida ni haki yangu kuchukizwa sana kwa yeyote kujaribu kunitukana kwa sababu yoyote ile!!! - hata kama kwa maoni yake nimejitakia au kujijengea mazingira ya kutukanwa!
AND by the way; hivi rafiki wa kweli; akikuona zipu imeteremka anakuzomea au unakuita chemba kukukumbusha ufunge zipu yako kufunika utupu?
Heri ya mwaka mpya bro
Edmond