Thursday, October 20, 2011

BREAKING NEWS: GADAFFI IS DEAD!

Gadaffi during his Glory Days
Former Libyan leader Muammar Gaddafi died of wounds suffered on Thursday as fighters battling to complete an eight-month-old uprising against his rule overran his hometown Sirte, Libya's interim rulers said.


His killing, which came swiftly after his capture near Sirte, is the most dramatic single development in the Arab Spring revolts that have unseated rulers in Egypt and Tunisia and threatened the grip on power of the leaders of Syria and Yemen.


"He (Gaddafi) was also hit in his head," National Transitional Council official Abdel Majid Mlegta told Reuters. "There was a lot of firing against his group and he died." REUTERS

TANESCO Walimuhujumu Lowassa Jana???


Wakati tukiendeleea kutafakari haya na yale katika hotuba ya Lowassa ya jana, mi nimekuwa na tafakari nyingine binafsi - KUKATIKA KWA UMEME!


Kwa siku kadhaa sasa, kumekuwa na hali stable ya upatikanaji wa umeme, kiasi cha watu wengi kufikia hatua ya kudhani Mgao wa Umeme umeisha - HAUJAISHA! Hali hiyo ilibadilika ghafla jana.


Baada ya juzi kutangaza kuwa Lowassa ataongea na Waandishi wa Habari jana jimboni kwake Monduli, ghafla mtaani kwetu nilishuhudia matatizo ya umeme kuanzia usiku wa kuamkia jana, umeme ulikuwa unakatika-katika ovyo usiku kucha, Asubuhi ukakatika na HAUKURUDI TENA.


Binafsi nilidhani ni tatizo la mtaani kwetu, lakini nilipotoka kwenda kazini na maeneo mengine nilikuta maeneo mengi hayakuwa na umeme mchana kutwa - na yaliyokuwa na umeme mchana USIKU UKAKATWA - mda ambao ndio wengi huutumia kupata habari mbalimbali baada ya kazi kupitia TV na Redio!


Nikiunganisha uhusika wa Lowassa katika suala la Umeme, Uhusika wake katika Siasa za Sasa Tanzania na uwezo na ujasiri wake katika kuzungumzia maswala mbalimbali bila kuuma mdomo wala kuogopa mtu, nikahisi kulikuwa na makusudi.


Kitendo kile kiliwapotezea "timing" watu wengi sana kuweza kupata zile taarifa kwa wakati - hususa - kwa wakati mmoja na mapema, kitu ambacho huwa ni muhimu na hatari sana katika uenezaji wa habari na harakati ya kujikusanyia wafuasi.

CCM: HOTUBA YA LOWASSA Monduli!

Edward N. Lowassa

HOTUBA YA MBUNGE WA MONDULI, EDWARD LOWASSA 
KWA WAANDISHI WA HABARI MONDULI, OKTOBA 19, 2011
NDUGU wana habari nimewaita katika mkutano huu leo kwa sababu moja kubwa, kutoa ufafanuzi kuhusu matukio ambayo yamekuwa yakitokea huku yakinihusisha mimi binafsi kwa namna ambayo sasa yanatishia ustawi na mshikamano wa kimaadili, kihistoria na kikazi miongoni mwa viongozi na baina ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ndugu wana habari, naamini mmkekuwa mkifuatilia kwa karibu habari zinazoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari  zinazolihusisha jina langu na harakati kadha wa kadha chafu ambazo hata mimi mwenyewe ninayehusishwa nazo huwa nazisikia na kuzijua baada ya kuwa zimesharipotiwa katika vyombo vya habari.

Uamuzi wangu wa kukutana nanyi leo hauna makusudi ya kuzozana na vyombo vya habari wala kwenda kinyume na utamaduni wa kimaadili wa ndani ya chama changu unaotutaka viongozi kujadili masuala yanayokihusu chama chetu ndani ya vikao vyetu rasmi vya kimaamuzi bali kutoa ufafanuzi na angalizo kwa pande zote hizo mbili ambazo zinaguswa na matukio yanayoendelea kutokea leo hii.

Moja ya mambo ambayo yameligusa jina langu kwa namna hiyo ni lile linalonihusisha eti na kundi moja la wanasiasa ambao wamekuwa na mikakati ya kumhujumu mwenyekiti wetu wa chama, Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete. Hakuna shaka ni madai ya kipuuzi, kizushi na yenye malengo machafu.

Hawakuishia hapo sasa wamefikia hatua ya kuvitumia vyombo hivyo hivyo vya habari kufikia hatua ya kudai kwamba nimeanza kuandaa orodha ya kile wanachokiita madhambi ya Rais Kikwete ambayo wandai nimepanga kuyasoma wakati wa kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (CCM).

Ninaamini kwa dhati kabisa kwamba, waandishi wa habari wanaofuatilia kwa karibu na kwa umakini mwenendo wa masuala ya kisaiasa nchini wanatambua kwamba, watu wanaopenyeza taarifa hizi katika vyombo vya habari wanafanya hivyo kwa malengo ya kufikirika na kujisafishia njia kisiasa.

Ni jambo lisiloingia akilini kunihusisha na kile kinachoitwa mikakati ya kumhujumu rais au chama ambacho mimi ni kada wake wa muda mrefu, mbunge anayetokana na chama hicho hicho na mtu anayeiongoza Kamati nyeti ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na zaidi ya yote kiongozi wa ngazi mbalimbali za kisiasa na kiserikali nilizowahi kushikilia.

Kuhusu hili napenda kusema kwa uwazi kwamba, mbali ya ukweli kuwa sijapata kufikiria hata mara moja kuhusu hicho wanachokiita mabaya au madhambi ya rais, sina wala siijui hiyo wanayoitaja kuwa ni orodha ya mabaya ya namna yoyote dhidi ya Rais Kikwete.

Mbali ya ukweli kwamba huo ni uongo wa wazi, silika yangu kama mwanasiasa na mtu mwenye dhamana kubwa kwa watu wa Monduli na kwa taifa langu haiwezi kamwe kunituma nianze kupanga mikakati ya kumhujumu kiongozi wetu mkuu au chama ambacho kimenilea na mimi mwenyewe nikakitumikia kwa uadilifu na kwa juhudi kubwa pengine kuliko ilivyo kwa hao wazushi.

Ndugu wana habari, nitakuwa ni mtu wa mwisho kufikiria au kupanga kumhujumu mwenyekiti wetu wa chama na rais ambaye nimemuunga mkono kwa dhati kwa muda mrefu na kushirikiana naye katika harakati nyingi za kifikra na za kiuongozi katika ngazi mbalimbali na kwa miaka mingi. Nilipatana kuliesema hili na leo nalirudia tena. Mimi na Rais Kikwete hatukukutana barabarani.

Tangu serikali ya Awamu ya Nne iingie madarakani kuna kundi la watu limekuwa likifanya juhudi kubwa kunigombanisha na Rais wakitumia kila aina ya hoja za kupikwa.

Kundi hilo ambalo sasa limekuja na uzushi mpya, ndilo ambalo mwaka juzi lilipenyeza ndani ya chama chetu na katika jamii hoja kwamba nilikuwa nimejipanga kugombea urais kwa tiketi ya chama chetu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, likidai kwamba nilikuwa na mlango ya kumpinga Rais Kikwete ambaye wakati huo alikuwa ndiyo kwanza anaelekea kukamilisha ngwe yake ya kwanza madarakani.

Katika kuthibitisha kwamba watu hao walikuwa na hila, nilipohojiwa na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam miezi kadha kabla ya Uchaguzi Mkuu nilijibu kwa kifupi nikisema, hatukukutana na Rais Kikwete barabarani.

Nayasema haya na kurejea baadhi ya mambo huku nikiwa na imani ya dhati kabisa kwamba, viongozi wenzangu ndani ya CCM na wale walio na nia njema na chama chetu na taifa hili, akiwapo Mwenyekiti wetu wa Taifa, Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete hawawezi kamwe kuamini kushawishiwa na propaganda chafu zinazoendeshwa na kikundi kidogo cha wanasiasa hao kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ambayo malengo yao ya kisiasa yako wazi na yanayojulikana.

Kama hiyo haitoshi, wanasiasa hao hao baada ya kulitumia jina langu kama ajenda yao ya uzushi wa kila  namna, sasa wameanza kunihusisha  hata na matukio ya kisiasa kama yale yaliyotokea majuzi tu hapa Arusha.

Ndugu wana habari baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu sasa, nimeamua kuanza kuchukua hatua mbalimbali za kisiasa na kisheria ambazo namini zitatoa majibu sahihi dhidi ya wale wote walio nyuma ya ajenda hizi chafu kwa lengo la kuweka kumbukumbu sawia ndani ya chama changu na kwa jamii nzima ya Watanzania ambao kwa muda mrefu wamelishwa mambo mengi ya kizushi na wakati mwingine ya hatari dhidi yangu.

Tayari nimepanga kuanza kuwasiliana na kuwasilisha malalamiko yangu kwa mamlaka husika zinazosimamia mienendo ya kimaadili na weledi wa kitaaluma wa vyombo vya habari kama vile Msajili wa Magazeti na Baraza la Habari Tanzania.

Kama hiyo haitoshi, baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu nimeshaanza kufikiria na kujipanga kuanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa habari na wahariri ambao kwa makusudi wameamua kutumia vibaya uhuru wa habari ambao serikali imeutoa. Naamini sote tunakubaliana kuwa; ‘UHURU USIO NA NIDHAMU NI FUJO.’

Ndugu zangu wana habari napenda kutumia furasa hii kutoa wito kwa viongozi wa chama na wale wa serikali kumsaidia  rais na chma chetu kwa kutimiza ipasavyo wajibu wao badala ya baadhi yao tena wakiwamo wale wenye dhamana nyeti kuwa vinara wa kutunga mambo ya kufikirika kama haya wanayofanya leo.

Viongozi wenye mawazo ya namna hiyo wanapaswa kutambua kwamba, muda adhimu wanaoutumia kubuni na kuzusha uongo kila kukicha mbali ya kuwavunjia heshima wao weneywe unavidhalilisha vyombo vya dola ambavyo vinafanya kazi kubwa kuhakikisha hujuma za namna yoyote dhidi ya viongozi na taifa zinadhibitiwa.

Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge na mtu aliyepata kuwa Waziri Mkuu ninatambua na kuiheshimu kwa dhati kazi hiyo kubwa inayofanywa kwa weledi mkubwa na taasisi mbalimbali za dola zenye wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama wa viongozi wetu na taifa kwa ujumla.

Ndugu wanahabari nazungumza nanyi baada ya kurejea nikitokea katika nchi za Nigeria, Malaysia, Singapore, India, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambako nilipata fursa ya kujifunza mambo mengi lakini moja muhimu likiwa ni namba vyombo vya habari (kwa maana ya waandishi wa habari) na wanasiasa wanavyotumia muda wao mweingi kujadili amasuala yanayogusa maisha na maendeleo ya watu wao.

Tofauti na kile wanachofanya wenzetu hapa nyumbani, ninyi wanahabari na sisi wanasiasa tumekuwa tukitumia muda wetu mwingi kujadili watu na propaganda za kisiasa zisizo na tija wakati tukitambua kwamba, taifa linakabiliwa na changamoto nyingi kama zile za kuhamasisha uwezekazji wa ndani na nje ya nchi, kuimarisha mifumo ya utawala bora, kuporomka kwa thamani ya shilingi kila kukicha, mdororo wa uchumi, tatizo kubwa la ajira kwa vijana, kushuka kwa kiwango cha elimu na ugumu wa maisha kwa ujumla. TUNAPASWA KUJISAHIHISHA.

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA

Tuesday, October 18, 2011

KIKWETE Ang'olewe Uenyekiti CCM!

Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete
Habari za siku kadhaa wadau...


Kuna sakata kubwa lingine - kati ya mengi - yanayoendelea ndani ya Chama changu cha Mapinduzi CCM. Sakata lenyewe linahusiana na fununu za kuwepo kwa "kundi" linalotaka Kikwete avuliwe Uenyekiti wa Chama na aendelee tu na nafasi ya Urais. Leo, natoa maoni yangu kuhusiana na suala la Mtu kuwa Rais na Mwenyekiti wa Chama tawala kwa Wakati mmoja.


Tangu enzi za Mkapa (ndipo nilipoanza kufuatilia Siasa kwa jicho la kutafuta kuelewa na uchambuzi), Msimamo na ushauri wangu mara zote ulikuwa RAIS HAPASWI KUWA MWENYEKITI WA CHAMA TAWALA! Sababu nitakayoijadilia mimi hapa ni moja na ambayo kwa hoja yangu ndiyo ya msingi: Uwajibikaji


Wakati chama kinapokuwa kinajiandaa kuingia kwenye Uchaguzi wowote, huwa kinatengeneza Ilani. Ilani hii kwa kawaida ndiyo huja kuwa mwongozo wa Chama wa utekelezaji baada ya uchaguzi na chama kinapokuwa kimeshinda uchaguzi.


Kwa hali hiyo, Mgombea wa Urais/Rais hukabidhiwa dhamana na Chama kuongoza utekelezaji wa Ilani. Kwa maana hiyo, Rais atatakiwa kuwa anakuja kwenye Chama kutoa taarifa za maendeleo ya utekelezaji wa Ilani, kuhojiwa, kurekebishwa, kuelekezwa, kukemewa, kurudiwa na hata kuadhibiwa iwapo kuna makosa au uzembe alioufanya au uliofanyika chini ya dhamana yake akiwa kama mwakilishi wa chama katika kutekeleza Ilani.
Kikwwte "akitumia" madaraka yake ya Urais
Tunapokuwa na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama tawala, unabaki na maswali makuu yafuatayo:


Ni nani anayeitisha vikao kujadilia maendeleo ya utekelezaji wa Ilani? Ni Nani anayeandaa ajenda za Mikutano? Ni nani anayeandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji? Taarifa inawasilishwa kwa Nani? Nani anayeongoza mjadala wa Taarifa ya utekelezaji, ukosoaji, mapendekezo na makemeo kwa Rais pale alipokosea? La mwisho na kubwa zaidi: NI NANI ANAYEMUADHIBU RAIS PALE ANAPOKUWA HAJATEKELEZA ILANI YA CHAMA KAMA INAVYOTAKIWA????? n.k.


Ukiyatafakari haya maswali yote kwa mtazamo wa kiutawala bora na uwajibikaji, utaona kuwa milango ya kufanyika mambo hayo yote kwa kufuata misingi ya utawala bora na uwajibikaji katka taasisi IMEFUNGWA - kwa sababu Mtoa Taarifa Ndiye Mpokea Taarifa na ndiye anayesimamia mijadala ya kujadili taarifa yake - ukiachilia mbali kwamba ndiye anayeandaa ajenda!
Kikwete "akitumia" madaraka yake ya kichama
Sababu za Kuunganisha Vyeo Hivi


Njia hii ya kumfanya Rais kuwa ndiye Mwenyekiti wa chama ilianza tangu wakati wa Nyerere na imekuwa ikifanyika hivi kwa miaka yote na katika nchi nyingi sana Afrika. Lengo lake kuu huwa ni kumpatia Rais madaraka juu ya Chama na Serikali kwa wakati mmoja na kwa namna hiyo kupunguza au kuondoa uwezekano wa chama kuweza kumgeuka na kumwajibisha kinyume cha vile atakavyo yeye.


Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa utaratibu huu umewekwa sio kwa ajili ya manufaa ya chama na taifa bali kwa maslahi ya Rais mwenyewe ili aweze kujihakikishia "usalama" wake awapo madarakani - kwa kukalia viti vyote viwili na kuwa na kauli kubwa katika nafasi zote hizo nyeti.


Upungufu wa Mfumo Huu


Utaratibu huu wa kumfanya Rais kuwa Mwenyekiti wa Chama haukuanzishwa kwa ajili ya kujenga na kuimarisha utawala bora na uwajibikaji katika Chama na serikali bali kwa ajili ya kumpatia nguvu Rais ya kusimamia Chama na Serikali kwa wakati mmoja. Hii inamuwezesha Rais kuweza ku-dictate maamuzi na matendo ya Serikali na ya Chama kwa wakati mmoja.


Utaratibu huu unaminya na kuziba mianya ya watu kuweza kuhoji na kuchukua hatua za uwajibishaji - hususan kwa upande wa Chama - kutokana na kutokuwa na nafasi "huru" ya kumchunguza, kumpima na kumhoji Rais juu ya Matendo yake katika kuitekeleza ilani, katiba na maamuzi ya Chama.


Matokeo ya "Uhodhi" huu


Matokeo yake huwa ni kwamba katika kila muda/awamu ya Utawala, sura na mwelekeo wa Chama huonekana kubadilika sana ku-akisi zaidi picha ya Mwenyekiti na Rais aliyepo madarakani zaidi kuliko sera, ilani na mwelekeo wa Chama kwa ujumla kama ulivyo kwenye "makaratasi". Sote ni Mashahidi kuwa CCM ya Nyerere, haikuwa ya Mkapa na haikuwa ya Kikwete (sijamtaja Mwinyi kwa makusudi).


CCM ya Nyerere kwa wale tunaoikumbuka vizuri, iliakisi zaidi falsafa, mitazamo na dira ya Nyerere kama Nyerere, vivyo kwa Mkapa na hatimaye kwa Kikwete. Mafanikio mengi na matatizo mengi yaliyokuwa yanatokea chini ya Nyerere, Mkapa na Kikwete (na namna yalivyo/yanavyo shughulikiwa) yanaakisi zaidi Uwezo, Utashi na mwelekeo wa Rais na Mwenyekiti kuliko  Chama kama chama.


Ili kuficha mapungufu na udhaifu wa viongozi wahusika, watu wengi hupenda kuhusianisha tofauti za tawala hizo na kile ambacho hudai kuwa ni "changamoto tofauti" zilizowakabili viongozi husika.


Madhara ya Kugawanya Madaraka


Kuna nchi moja jirani - Malawi - ambako ilitokea Rais HAKUWA mwenyekiti wa Chama tawala. Katika mchakato wa kuwajibishana, kulitokea hali kubwa ya kutokuelewana baina ya Mwenyekiti wa Chama tawala na Rais kiasi cha kupelekea chama kugawanyika. 


Mwisho, Rais alijiengua kwenye Chama tawala na akaanzisha Chama chake kingine na kuondoka na baadhi ya wafuasi kutoka Chama tawala. Katiba yao inawaruhusu kufanya hivyo na kuendelea kushikilia madaraka ya Urais! Kuna mifano mingi ya namna hii katika mataifa mengi.


Nini Kifanyike


Kwa hapa Tanzania, umekuwa ni ushauri wangu tangu zamani kwamba Rais ASIWE mwenyekiti wa Chama. Hii itasaidia uwepo wa mwenyekiti na uongozi tofauti katika chama kuweza kufuatiliana na kutaathimini kwa karibu utendaji wa Rais katika kutekeleza ilani ya Chama na kuweza kumshauri, kumuonya, kumkemea na hata kumuadhibu kisiasa ndani ya chama.


Hoja yangu hii inatiwa nguvu zaidi na jinsi ambavyo Rais wetu wa Sasa Kikwete J. M. ameonesha uwezo mdogo sana wa kukimudu chama tawala na Serikali kwa wakati mmoja. Changamoto nyingi sana zimeibuka chini ya utawala wake ndani ya chama na kitaifa kwa ujumla. 


Changamoto hizi zilikuwa fursa kubwa sana kwake kuweza kutumia vizuri hizo kofia mbili ya kuthibitisha kwamba alistahili kuwa nazo zote - lakini kwa bahati mbaya ameonesha kushindwa kwa kiasi kikubwa sana.


Nashauri Kikwete aachie au anyang'anywe (kama hayuko tayari kuachia) Nafasi ya Uenyekiti wa Chama ili kutoa nafsi kwa mtu mwingine kukisimamia Chama katika shughuli zake za kila siku na yeye abaki na madaraka ya urais kwa ajili ya kutekeleza ilani na awe anatoa ripoti na kuwajibika kwa Chama kilicho chini ya mwenyekiti ambaye sie yeye - na utaratibu huu uendelee hivyo kwa wagombea na Marais wajao - bila kujali chama.


Naamini mgawanyo huu utasaidia kuongeza ubora wa utendaji na uwajibikaji - japo pia kunaweza kuwa na hatari za mgawanyiko kama ilivyotokea Malawi.


Wasaalam.... //msb


N.B: Maoni haya ni yangu binafsi, yaliyojengwa katika ufahamu wangu wa masuala ya siasa na utawala na hayahusiani na kundi au kambi zozote ndani ya chama changu cha mapinduzi.

Saturday, October 15, 2011

MAUAJI IGUNGA: MAITI Zaidi Zaokotwa!

Taarifa Hii Nimeipokea kama ilivyo hapa chini Kupitia Mtandao wa Wanabidii na Iliandikwa na Fredrick Katulanda.


"Maiti za wanawake wawili zimeokotwa jana katika msitu wa kijiji cha Ulaya, Kata ya Nkinga wilayani Igunga zikiwa zimeharibika vibaya.

Wakati uchunguzi unaendelea, taarifa za awali zinaeleza kuwa mmoja wao ambaye ni
mama wa makamo, anajulikana kuwa ni shabiki mkubwa wa Chadema na Mhamasishaji maarufu mwenye ushawishi wa kisiasa, alikuwepo siku Helikopta ya CHADEMA ilipotua Nkinga na Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa ajili ya kampeni siku ya J'4 kabla J'2 ya uchaguzi, Baada kumalizika mkutano huo muda wa jioni sana, mama huyo alikuwa akirudi kijijini kwake, lakini kuna kikundi cha vijana wa makambi wa CCM walionekana wakimfuatilia, wakiwemo watoto wawili wa Diwani wa kata hiyo ambao ni maarufu kwa ujambazi lakini mara zote wanakingiwa kifua na baba yao kwa wadhifa wake wa udiwani, mama huyo hakuonekana tena
hadi maiti yake ilipookotwa jana msituni ikiwa bila nguo (zimetundikwa juu ya mti) na imeharibika vibaya na kuliwa na wadudu
.

Upande wa pili wa barabara alipookotwa mama huyo kulikutwa maiti nyingine ya mwanamke mwingine aliyeuawa kwa staili ileile na kuachwa bila nguo, ila kutokana na kiwango cha kuharibika kwake inaelekea
aliuawa siku tofauti na kuja kutupwa hapo, pembeni yake wauaji hao waliweka kitambulisho cha mtu wanaetaka ahusishwe na mauaji hayo, dalili zote zinaonesha wauaji ni walewale, inasemekana mwanamke huyo ametokea kata jirani ya Ndembezi.

Polisi zaidi ya kuchukua maiti hizo kwa pamoja na kuondoka nazo haijasema lolote, jitahada kubwa zinafanywa kulifunika suala hili liishe kimyakimya lisije likaleta kashfa kubwa ya mauaji kwa chama
tawala, baada ya Nape Nauye kuahidi kuwa watafanya hivyo na wasilaumiwe kwa kuwa kuna kijana wao amemwagiwa tindikali.

Inaelekea kuna maiti nyingi zaidi hazijapatikana maporini na nyingine zimefukiwa huku ndugu zao wakidhani wamesafiri au wako kwenye mihangaiko, lakini kwa kuwa La Kuvunda Halina Ubani, basi kitaeleweka tu!"