Saturday, October 15, 2011

MAUAJI IGUNGA: MAITI Zaidi Zaokotwa!

Taarifa Hii Nimeipokea kama ilivyo hapa chini Kupitia Mtandao wa Wanabidii na Iliandikwa na Fredrick Katulanda.


"Maiti za wanawake wawili zimeokotwa jana katika msitu wa kijiji cha Ulaya, Kata ya Nkinga wilayani Igunga zikiwa zimeharibika vibaya.

Wakati uchunguzi unaendelea, taarifa za awali zinaeleza kuwa mmoja wao ambaye ni
mama wa makamo, anajulikana kuwa ni shabiki mkubwa wa Chadema na Mhamasishaji maarufu mwenye ushawishi wa kisiasa, alikuwepo siku Helikopta ya CHADEMA ilipotua Nkinga na Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa ajili ya kampeni siku ya J'4 kabla J'2 ya uchaguzi, Baada kumalizika mkutano huo muda wa jioni sana, mama huyo alikuwa akirudi kijijini kwake, lakini kuna kikundi cha vijana wa makambi wa CCM walionekana wakimfuatilia, wakiwemo watoto wawili wa Diwani wa kata hiyo ambao ni maarufu kwa ujambazi lakini mara zote wanakingiwa kifua na baba yao kwa wadhifa wake wa udiwani, mama huyo hakuonekana tena
hadi maiti yake ilipookotwa jana msituni ikiwa bila nguo (zimetundikwa juu ya mti) na imeharibika vibaya na kuliwa na wadudu
.

Upande wa pili wa barabara alipookotwa mama huyo kulikutwa maiti nyingine ya mwanamke mwingine aliyeuawa kwa staili ileile na kuachwa bila nguo, ila kutokana na kiwango cha kuharibika kwake inaelekea
aliuawa siku tofauti na kuja kutupwa hapo, pembeni yake wauaji hao waliweka kitambulisho cha mtu wanaetaka ahusishwe na mauaji hayo, dalili zote zinaonesha wauaji ni walewale, inasemekana mwanamke huyo ametokea kata jirani ya Ndembezi.

Polisi zaidi ya kuchukua maiti hizo kwa pamoja na kuondoka nazo haijasema lolote, jitahada kubwa zinafanywa kulifunika suala hili liishe kimyakimya lisije likaleta kashfa kubwa ya mauaji kwa chama
tawala, baada ya Nape Nauye kuahidi kuwa watafanya hivyo na wasilaumiwe kwa kuwa kuna kijana wao amemwagiwa tindikali.

Inaelekea kuna maiti nyingi zaidi hazijapatikana maporini na nyingine zimefukiwa huku ndugu zao wakidhani wamesafiri au wako kwenye mihangaiko, lakini kwa kuwa La Kuvunda Halina Ubani, basi kitaeleweka tu!"

No comments:

Post a Comment