Kwa siku kadhaa sasa, kumekuwa na hali stable ya upatikanaji wa umeme, kiasi cha watu wengi kufikia hatua ya kudhani Mgao wa Umeme umeisha - HAUJAISHA! Hali hiyo ilibadilika ghafla jana.
Baada ya juzi kutangaza kuwa Lowassa ataongea na Waandishi wa Habari jana jimboni kwake Monduli, ghafla mtaani kwetu nilishuhudia matatizo ya umeme kuanzia usiku wa kuamkia jana, umeme ulikuwa unakatika-katika ovyo usiku kucha, Asubuhi ukakatika na HAUKURUDI TENA.
Binafsi nilidhani ni tatizo la mtaani kwetu, lakini nilipotoka kwenda kazini na maeneo mengine nilikuta maeneo mengi hayakuwa na umeme mchana kutwa - na yaliyokuwa na umeme mchana USIKU UKAKATWA - mda ambao ndio wengi huutumia kupata habari mbalimbali baada ya kazi kupitia TV na Redio!
Nikiunganisha uhusika wa Lowassa katika suala la Umeme, Uhusika wake katika Siasa za Sasa Tanzania na uwezo na ujasiri wake katika kuzungumzia maswala mbalimbali bila kuuma mdomo wala kuogopa mtu, nikahisi kulikuwa na makusudi.
Kitendo kile kiliwapotezea "timing" watu wengi sana kuweza kupata zile taarifa kwa wakati - hususa - kwa wakati mmoja na mapema, kitu ambacho huwa ni muhimu na hatari sana katika uenezaji wa habari na harakati ya kujikusanyia wafuasi.
No comments:
Post a Comment