Nilipoipokea hii post hapa Chini kwenye Email yangu, iliamsha hamu yangu ya kufahamu haya maandalizi ya Sherehe za Uhuru yataligharimu taifa kiasi gani Cha fedha??
Kwa bahati mbaya sana nina experience mbaya ya Matumizi ya fedha za Umma kwenye sherehe au matukio mbalimbali. taarifa zinaonesha kuwa MABILIONI KWA MABILIONI hutumika kwa kuandalia Sherehe mbalimbali ambapo watu wengi hulipwa Posho pamoja na manunuzi yenye gharama kubwa.
Ninaomba kama kuna Mtu ana taarifa japo za mfano kutoka Wilayani, Mikoani au hata kwenye Wizara / Taifa kuhusiana na Bajeti mbali mbali ambazo zimetengwa kwa ajili ya "Sherehe" hizi. Tayari naona matumizi makubwa ya fedha kwenye "Vipindi Maalum" vya Televisheni taasisi zikijisifu kwa jinsi zilivyo "thubutu, weza na kusonga mbele"....
Mwenye taarifa na takwimu tafadhari!
"Wapendwa wana AZAKI napenda kueleza dukuduku langu juu ya nilichosikia na kushuhudia katika maadhimisho ya sherehe ya miaka 50 ya Uhuru wa TZ.Kwa kweli kinacho fanyika ni ULAJI MTUPU.Habari nilizo zipata ni kwamba viongozi walio alikwa kwenye sherehe hizi hapa kwetu Iringa ni LUKUKI.
Kila Wilaya imeleta wakuu wa idara ambao kwa kawaida ni idara 12 mara wilaya zetu saba unapata 84,Wakuu wa Wilaya 7,Wakurugenzi 7,Hawa nikutoka wilayani.Bado wale wa Idara za Mkoani,Wanajeshi,Usalama wa Taifa,TakukuruWenyeviti wa Halmashauri toka Halmashauri 7,wenyeviti na makatibu wa CCM wa wilaya 7.Jumlisha madereva,na kama unavyo jua wa TZ kila BOSI anataka kuja na gari lake,Ndiyo, atajulikanaje?
Hawa wote kwa jiji tarajiwa la Iringa wana lipwa posho ya tsh 80,000/=achana na MATUPUTUPU kama sio Maluplupu mengine.Ni sherehe ya siku karibu tano hivi.Ukipiga hesabu za darasa la tatu,ni mamilioni.Wakubwa hawa wana kula na kunywa kuadhimisha miaka 50 ya kushindwa kuwaondoa maadui wale ambao aliwaacha mkoloni miaka hamsini,UJINGA,UMASIKINI NA MARADHI.
Wakubwa wanajipongeza kwa hayo.Hakika ni aibu sana,katika hospitali zetu hakuna dawa,shuleni hakuna madawati walavitabu,Hivi kweli tuna sababu ya kujisifia?
Oneni mambo haya wana AZAKI.Nyuma yake msafara wa mwenge nao unakula mapesa ya walala hoi.Mungu ibariki Tanzania,tubariki wanyonge wote,ili siku moja tuwapate viongozi wenye uchungu na wananchi wao na watetea haki.
Nawatakia kazi njema."
Severin mtitu
mkurugenzi-ADG.
Box 1002.
Iringa.
No comments:
Post a Comment