Wednesday, November 9, 2011

USHOGA: Poleni Mliomsifu KIKWETE!

Siku Moja tu Baada ya Serikali ya Tanzania
Kutoa Tamko "Kali" Dhidi ya Serikali ya Uingereza,
Mwana-Mfalme wa Uingereza Anapewa
Mapokezi ya Heshima Kabisa na RAIS WETU!!

Jana katika tafakari yangu kuhusiana na Sakata la Tanzania kutakiwa kuruhusu Ushoga ili iendelee kupokea misaada kutoka Uingereza, nilielezea kwa ufupi ni kwa kiasi Gani Sera KUOMBA-OMBA MISAADA za Rais wetu KIKWETE zimachangia kulifikisha taifa kwenye hali hii.

Siku chache baada ya kauli ya David Cameron, Waziri Mkuu wa Uingereza, kutishia kusitisha misaada, Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya Nje Membe iliirukia hiyo fursa na kutaka kuitumia kutunisha misuli kwa Wazungu. 

Kauli ya Membe ilijawa na kauli zenye kuonesha Ujasiri, Msimamo, Kutokuyumbishwa, Uhuru wa Taifa na mbwembwe nyingi ambazo mtu yeyote anatarajia kuzikuta kwenye hotuba ya Kiongozi wa Nchi wa Maskini anayetaka kuonekana kwa wanachi wake kuwa ni Maskini Jeuri!

Namfaham KIKWETE wa DOWANS...!
Tarehe 5/februari/2011 kwenye maadhimisho ya miaka 34 ya CCM, Kikwete wakati akihutubia alitoa kauli ambazo kwangu HAZIKUFAA kutoka kwa kiongozi wa taifa. Kwa ufupi, alitoa kauli ya kukana kata-kata kuwajua wamiliki wa DOWANS! 
Akihutubia Wana-CCM Dodoma, KIKWETE alikana kuwajua DoWANS,
siku Chache baadaye ALIMKARIBISHA IKULU MMILIKI WA DOWANS
 MPYA (Symbion Power)!!!

Kauli hii, kwa wananchi wengi ambao hawamjui Kikwete ninayemjua mimi, walishangilia na kuichukulia kama kauli inayomaanisha Kikwete hahusiki kwa namna yoyote na DOWANS (japo hata kwa Uzembe tu)!

Miezi michache baadaye, nikiwa safarini kuelekea Iringa, nilinunua Gazeti moja na kukuta Picha kubwa ya rais Kikwete akiwa IKULU amekaa anazungumza na kucheka na Mmiliki wa Kampuni ya Symbion Power (AMBAYO NDIYO ILINUNUA MITAMBO NA MKATABA WA DOWANS)!!!!!!!!!!!!

Serikali Yaipinga Uingereza!
Baada ya tamko la Serikali kupinga "vikali" kauli ya waziri Mkuu wa Uingereza, Viongozi wa Dini mbalimbali walimimina Salaam nyingi za pongezi kwa Serikali kwenye makongamano yao ya Sherehe na Ibaada! 

Taarifa za Vyombo vya habari siku ya Idd, kwa mfano, zilifunikwa na Pongezi za Masheikh kwa Serikali kwa kupinga Ushoga! Maaskofu na Mapdre hawakuwa nyuma katika "mbwembwe" hizo pia za "kuipongeza" serikali - HAWAIJUI Serikali yetu, labda!

Mfalme wa "Ushoga" Atinga Ikulu!
Kama ilivyotokea kwa DOWANS na hatimaye Symbion Power, Siku moja tu Baada ya Wananchi kuimiminia Serikali Pongezi nyingi kwa kauli yake dhidi ya Ushoga, SIKUAMINI MACHO YANGU KUMUONA KIKWETE YUKO PRINCE CHARLES WA UINGEREZA, IKULU, DAR ES SALAAM!!!!!!!!!!!!!!!!!
Muda Mfupi baada ya Serikali "Kuikoromea" Uingereza,
Ni tabasamu na Vicheko IKULU, KIKWETE na
Mwana-Mfalme wa Uingereza!!!!!!!!!!!!!!!
Kitendo hakikunishangaza sana kwa jinsi ambavyo tayari namfaham Kikwete, lakini nilijua ni sawa na kofi la usoni kwa walimimina pongezi nyingi kwa Serikali siku moja kabla. Nilipouliza nikaambiwa tena SIO kwamba Prince Charles aliomba kuja Tanzania, BALI ALIALIKWA NA KIKWETE!!!!!!!!!!!!!!!

Iwapo ni kweli kauli ya Membe ilikuwa ina mashiko na nguvu kama ilivyodhaniwa wakati anaitoa kwa waandishi wa habari, basi ilikuwa ni dhahiri kwamba Tanzania ilikuwa imefikia katika hatua nzuri ya kuwaonesha Waingereza kwamba "haipelekeshwi" na masharti yao.

Kwangu mimi, safari hii ya Mwana Mfalme Charles hapa Tanzania ingekuwa ni fursa nzuri ya Serikali kuonesha kwamba imekasirishwa na kauli ya Cameron kivitendo. Hakuna kitendo ambacho kingeonesha kuwa Serikali imekasirishwa na hiyo kauli kama KUMZUIA Prince Charles ASIJE Tanzania hadi hapo baadaye.
kama kawaida, Mzungu akija kwa WATU MASKINI KAMA SISI
Lazima atoe msaada - japo wa  Vitabu - Hata kama Msaada
una thamani ndogo KULIKO CHAKULA TULICHOMLISHA SISI!!!
Mambo ya msingi ambayo serikali yetu ambayo ingeyafanya, iwapo ilikuwa serious na zile kauli za Membe, ni pamoja na kutaka Maelezo Rasmi ya kimaandishi kutoka kwa Serikali ya Uingereza kuhusiana na hiyo kauli au kuikanusha, na hata kuahirisha Ziara za Viongozi wa Uingereza hapa Tanzania hadi suala husika litakapokuwa limetolewa ufafanuzi na kueleweka vizuri kwa pande zote....!

IKAWA KINYUME....
BADALA YAKE Vicheko, hoi hoi, Nderemo na vifijo vilitawala Ikulu wakati Mwana Mfalme wa Uingereza alipotinga Ikulu ya Tanzania na kupokelewa na KIKWETE kwa tabasamu, furaha na amani yote ya moyo!!!

Kawaida, Hotuba fupi ikasomwa, sina uhakika ni nini kilikuwemo kwenye hotuba hii, lakini mara nyingi huwa zinakuwa na maelezo ya kueleza "shida" tulizo nazo na kuzitumia "KUOMBA MISAADA"...
Hotuba hizi mara nyingi hutumiwa kuelezea Shida
zetu katika nchi "maskini" kama Tanzania na kutumiwa Kuombea Misaada!
Poleni ambao hamuzifahamu Serikali za Afrika!
Nawapa pole wale wote ambao labda - kwa kujua au pasipo kujua - walikimbilia kuipongeza Serikali kwa kauli yake kuhusiana na Ushoga majuzi, kwa sababu hawakujua kuwa Serikali ya Tanzania ni sawa na serikali nyingi za Afrika - Inaongozwa na Watu ambao wanategemea sana MISAADA na wakati huo huo WANAPENDA SANA Kusifiwa na wananchi wao kuwa "Mashujaa" wa kupinga "Ukoloni Mambo leo" - japo kwa kauli tu....

Tanzania bila Misaada inawezekana, Japo sioni kama tuna viongozi Tanzania wanaoliona, kuliamini na kuliweka hilo kwenye vitendo......

5 comments:

  1. A stupid writer thinks can deceive people by these malicious, vague statements. Is admitting his visit a yes nodding to their demands of homosexality. Acha siasa za kipumbavu za kigomvi kama za cdm hapa. Kwani si wao walioweka sharti la kupewa misaada ni kukubali ushoga? Na nchi ikasema kama hilo ndiyo hitajio basi nendeni na misaada yenu..hatutaki hatudanganyiki..sasa yule aliyekukatalia akisema nakuja kukutembelea una haja gani ya kukataa? kwani kaja kufanya hiyo sodomy? Huwezi mshawishi yeyote labda bwege

    ReplyDelete
  2. wewe uliyopost maoni yako hapo nashukuru kwakuwa umeamua kuitusi chadema ila hatuna tabia ya kubishana na mashoga kama nyie ccm munao ona aibukujitangaza, atimwajitia wanaume huku kampaniyenu kubwa mashoga akina princ chars,ikulu iliandaa tafrija jakumshngilia shoga kuja ikulu nakugeuza ikulu yetu kuwa ya mashoga anaye tembea na shoga nayeye nishoga kwahito jk ni....?

    ReplyDelete
  3. nimesoma habari ya kumkaribisha mwanamfalme wa UK kwamba imekuwa ni kasoro kwa Kikwete kumkaribisha.nadhani watanzania mjitahidi kufanya tafiti hasa katika mifumo ya nchi za nje inavyokwenda naomba soma vyema siasa za uingereza zilivyo kisha ndio uandike makala yako.

    ReplyDelete
  4. Nadhani ungeenda moja kwa mja kwenye point na kueleza kipi kilipaswa "kusomwa" ingekuwa mchango mzuri zaidi pia.... Kusoma huwa hakuwafanyi watu wakaona na kutafsiri mambo kwa mtazamo mmoja, eleza wa kwako pia tujadili pamoja....

    ReplyDelete
  5. TANZANIA IMEOZA KWA KIFUPI KILA MTU ANANGALIA NA KUSHIKILIA PALE ALIPO HATUNA SERIKALI WALA NN SS HIVI KILA MTU ANAJIONGOZA MWENYEWE KWA MTU ANYEJUA DHAMANA YAKE KWA WATU WAKE HAKUPASWA HATA KWENDA AIRPORT KUMPOKEA BUT WE NEVER KNOW LABDA NDIYO ALIKUJA NA HUO MKATABA ILI WENYEWE WAMWAGE WINO NDIYO TUSHAKUBALI HIVYO USHOGA ME NAWAOMBA WALE WANAOFANYA MCHEZO HUO WAJITOKEZE TU KWA RAHA ZAO KWANI KWA SS HAMNA WA KUWASUMBUA TENA RUKSAA.

    ReplyDelete