Thursday, September 22, 2011

TGNP na USHOGA/USENGE: Shutuma Zazidi Kuongezeka!



Stanslaus Nyembea
Dar es salaam
                                                                                                                                     September 22, 2011
MTANDAO WA JINSIA TANZANIA-TGN
P.O.BOX P.o.Box 8921
Dar es Salaam
Tel: +255 22 2443450
TO WHOM IT MAY CONCERN
YAH: MAONI BINAFSI JUU YA HALI YA USHOGA NA TAMASHA LA JINSIA
Mimi ni miongoni mwa wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu, maliasili na mazingira. Nimekuwa nikipigania haki za kimsingi za kibinadamu kwa nadharia na vitendo. Ushiriki wangu umesaidia kupambana na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa namna moja au nyingine katika nchi yetu na nchi jirani.
Nitumie fursa hii kuipongeza kwa dhati kabisa Tanzania Gender Networking  Program (TGNP) kwa mchango wake wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii ya kitanzania. Mchango wa TGNP ni mkubwa na wanaharakati wa haki za binadamu, rasilimali na Mazingira kwa ujumla wanautambua na kuuthamini.
Baada ya pongezi hizi, napenda kutoa maoni yangu juu ya Tamasha la Jinsia liloandaliwa na TGNP kuanzia tarehe 13-16 katika viwanja vya TGNP.
Ni kweli kuwa kuna mambo mazuri mengi yalifanyika wakati wa Tamasha hili, ikiwemo jamii za pembezoni kutoa na kupaza sauti zao kuhusu masuala mbalimbali nyeti yanayozifanya jamii hizi kukosa au kunyimwa haki zao za  kimsingi za kibinadamu.
Pamoja na hayo mazuri, kwa maoni na mtizamo wangu, mazuri hayo yalifutwa kabisa na msimamo na upigiaji chapuo  wa TGNP kuhusu masuala ya USHOGA katika jamii ya kitanzania. Binafsi sikatai uwepo wa USHOGA/USENGE katika jamii ya kitanzania. Sina mtizamo wa kihafidhina wala wa kuwatenga watu hawa, lahasha. Tatizo langu ni kupigia chapuo kwa TGNP suala hili la USHOGA/USENGE.
Hoja yangu ya kupingana na TGNP kuhusu mtizamo wenu ni jinsi mlivyolichukulia na kulienzi suala hili. Nashindwa kupata dhamira nyingine zaidi ya kuwa TGNP mna malengo kadhaa na suala hili. Nashawishika kuamini kuwa mnapigania kuleta mabadiliko hasi kwa jamii yetu, yaani jamii ya kitanzania ilione suala hili kuwa la kawaida, hivyo watoto wetu wajihusishe na USHOGA/USENGE.
Pengine, utetezi wenu kuwa mnataka jamii ijue kuwa tatizo hili lipo na ichukue hatua. Lakini hoja hii haina mashiko wala miguu.
Utetezi wenu pia kuwa watu hawa, MASHOGA/WASENGE wameingia katika matendo haya machafu kwa sababu za kiuchumi na kibiojia nayo hayana maantiki hata kidogo.
Je, mbona masikini wa Tanzania wapo wengi tu! Na wao mnataka waingia katika USHOGA/USENGE? Je ukishakuwa SHOGA/MSENGE ndiyo matatizo ya kibiolojia na kiuchumi yanaisha? Nini mnataka watoto wetu wafanye zaidi ya kuona USHOGA ndiyo suluhisho la umasikini?
Je kama watoto wenu wangekuwa mashoga/wasenge mngewaleta kwenye tamasha hili?
Jibu rahisi ni kuwa TGNP mnapata fedha za kuwa na miradi hii toka kwa mashoga/wasenge wa kimataifa wanaotaka kufanya jamii nzima iwe kama wao. Ni tamaa ya fedha tu ndiyo inayowafanya mpigie debe suala la ushoga/ushoga nchini mwetu na si vinginevyo. Kuna tofauti gani kati ya RUSHWA/UFISADI mnaoukataa katika serikali yetu na kutumia fedha chafu za watetea USHOGA/USENGE. Fedha yao ni chafu, hata ikitumika kuutokommeza USHOGA bado itakuwa chafu tu.
Je, unaweza kutumia fedha ya mtetea USHOGA/USENGE kuwafanya mashoga waache tabia hii? Mbona haiwezekani! Lengo ni kuwatetea tu waendelee na tabia hii chafu na si vinginevyo.
Vile vile naona TGNP kupoteza staha na heshima iliyojijengea katika jamii yetu ya Tanzania kwa muda mrefu. TGNP kwa kujiingiza kwenye suala hili ni kupoteza dira na mwelekeo sahihi. Siwahukumu ila ndiyo ukweli mwenyewe. Mnataka tuwe na taifa la aina gani? La mashoga/wasenge? Ukuaji wa taifa utakuwaje ikiwa watu wote watakuwa kama dhamira ya wasenge ilivyo?
Uungwana huanzia nyumbani. Ikiwa matendo na sera zenu zitakosa staha kwa watanzania kazi yenu itakuwa ni mfu na isiyo na tija. Uungwaji mkono wenu wa kwaida utapotea sana.
Nawasihi mtafakari upya mwelekeo wenu ili heshima na staha yenu irudi kwa watanzania. Kuteleza siyo kuanguka, chukueni hatua hamjachelewa. Chukueni maamuzi magumu ya kukataa fedha za watetea USHOGA/USENGE. Zipo nyingi tu na ndizo zilizowaingiza katika mtego huu mchafu.
Stanslaus Nyembea

USHOGA na Wanaharakati wetu Tanzania!

Tamasha la Jinsia TGNP
Hivi karibuni lilifanyika na kukamilika tamasha la Jinsia Tanzania - kwa sababu kadha wa kadhaa - zikiwemo kubana kwa ratiba yangu sikuweza kuhudhuria. Kama kawaida, tamasha liliandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na Mashirika mengine, hususan yenye Ajenda ya masuala ya Jinsia au wananchama wa Mtandao wa FemAct.

TGNP ni Shirika linalotambuliwa sana
kwa kuongoza "Harakati za Wanawake"
Ushoga Kupamba Tamasha!
Taarifa ya kwanza kabisa niliyoipokea kutoka kwa mshiriki mmoja wa Tamasha hilo ni kile alichoeleza yeye kwamba Tamasha hilo LILIFUNIKWA NA MASHOGA! Kw amujibu wa maelezo yake mashoga hao walikuwa kama 30 hivi. Maelezo yake yalionesha kwamba mojawapo ya mambo yaliyopigiwa debe sana katika Tamasha hilo ilikuwa ni KUDAI HAKI ZA MASHOGA TANZANIA!


Tumeingiliwa kama Taifa!
Taarifa hizi binafsi hazikunishtua sana kwa maana naijua vizuri TGNP, lakini labda zaidi sana NAWAJUA VIZURI WALE WANAOJIITA WANAHARAKATI WA MASUALA YA "JINSIA"! Kilichonishtua mimi ni kwamba mambo ambayo "wanaharakati" wetu kwa kawaida wamekuwa wakiyasema, kuyatetea na kuyapigia debe katika majukwaa ya kimataifa, SASA WANAYALETA NYUMBANI!


Napinga Waziwazi!
Ukimya wangu katika Masuala mbalimbali yanayofanyiwa propaganda na kupigiwa debe na hawa wanaojiita kuwa ni "Wanaharakati wa Jinsia" sasa umefikia mwisho - BAADA YA WAO KUVUKA MSTARI! 


Binafsi nimekuwa nikipinga sana madai mengi yanayotolewa na hawa "wanaharakati" kwa sababu mengi SIO YA KWELI, MENGI NI YA UCHOCHEZI NA KUJENGA CHUKI BAINA YA WANAWAKE NA WANAUME KATIKA JAMII, MENGI (naamini) YANASUKUMWA NA AJENDA NA FEDHA ZA WAFADHILI - Ambao wengi ni Pro-Mashoga!
Ananilea Nkya ni mmoja wa wanaharakati wa masuala
ya "jinsia" Tanzania. Hapa akiongea na "wanaharakati"
kutoka Zimbabwe wakati wa Tamasha la Jinsia
Katika hatua nyingine, baada ya Shutuma kuanza kuibuka kwa kasi kuelekezwa kwa "wanaharakati" hawa, Mwanaharakati mmoja wao, Bi Ananilea Nkya alijitokeza na kuandika makala kuhusiana na USHOGA ambayo mimi niliisoma kupitia jukwaa la wanabidii.... Title ya Ile makala ilikuwa inatosha kabisa kukuelezea mtazamo wake kuhusu ushoga - ilisomeka: USHOGA  NI TUNDA YA MiFUMO MiBAYA.


Kwa kusoma tu hii title unaweza kuelewa wazi kwamba huyu mwandishi - IWAPO NI MTANZANIA - analenga mojamoja kwa kuepuka kushutumu ushoga na mashoga na badala yake anataka ieleweke kwamba ushoga na mashoga SIO TATIZO bali tatizo ni kile anachodai kuwa ni MFUMO!




Tuchukue Hatua!
Wito wangu kwa jamii yote ya Watanzania: tunapaswa kuamka sasa na kuanza kuwaangalia hawa wanaharakati wa masuala ya kijinsia kwa jicho la karibu na makini sana.


Uamuzi huu wa Watanzania wenzetu kuamua kujiunga na kutumia mashirika yao KUTETETA NA KUPIGIA DEBE USHOGA NA MASHOGA HADHARANI sio wa kupuuzwa wala kufumbiwa macho hata kidogo! Ni lazima tupinge UPUUZI HUU bila kujali unafadhiliwa au kusimamiwa na Nani!


TUSIONEANE AIBU WALA HAYA KATIKA HILI - TUPINGE USHOGA NA USAGAJI HADHARANI NA KWA NGUVU ZOTE.... Tanzania Bila Mashoga na Wasagaji Inawezekana - Tusiufiche UOVU NA USHENZI HUU kwenye kivuli cha Mfumo!!!!


...//msb

Thursday, September 15, 2011

WAKUU Wapya - Mikoa!


Kila nikiangaliaga uteuzi wa Kikwete huwa naona kama naiangalia Mv. Spice Islanders...!!!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA MIKOA WAPYA



RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa nchini.

Katika mabadiliko hayo, amewateua Wakuu wa Mikoa wapya 15, kuwabadilisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa watano na wengine saba wamestaafu kwa mujibu wa taratibu. Mkuu wa Mkoa wa Singida amebaki kwenye kituo chake cha kazi wakati Wakuu wa Mikoa wengine wanne watapangiwa kazi nyingine.

Aidha, Wakuu wa Mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika watatangazwa baadaye.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Wakuu wa Wilaya 11 wamepandishwa Vyeo na kuwa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo: Bw. John Gabriel Tupa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara; Bw. Saidi Thabit Mwambungu (Ruvuma); Bi. Chiku S. Gallawa (Tanga); Bw. Leonidas T. Gama (Kilimanjaro); Dk. Rehema Nchimbi (Dodoma); Bw. Elaston Mbwillo (Manyara); Kanali Fabian Massawe (Kagera); na Bibi. Fatma Abubakar Mwassa (Tabora). Wakuu wa Wilaya wengine walioteuliwa ni Bw. Ali Nassoro Rufunga, (Lindi); Eng. Ernest Welle Ndikillo, (Mwanza); na Bw. Magesa Stanslaus Mulongo Mkuu wa Mkoa (Arusha).

Walioteuliwa nje ya nafasi hizo ni Eng. Stella Manyanya (Rukwa); Bibi Mwantumu Mahiza, (Pwani); Bw. Joel Nkaya Bendera (Morogoro) na Bw. Ludovick Mwananzila (Shinyanga).

Waliobadilishwa vituo vya kazi ni Bw. Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza; Bw. Said Mecki Sadiki anayekwenda Dar es Salaam akitokea Lindi; Bibi Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma; Lt. Kanali Issa Machibya anayekwenda Kigoma akitokea Morogoro; na Kanali Joseph Simbakalia anayekwenda Mtwara akitokea Kigoma. Dk. Parseko Ole Kone ataendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Waliostaafu ni Bw. Mohammed Babu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera; Bw. Isidore Shirima aliyekuwa Arusha; Kanali (mst.) Anatory Tarimo aliyekuwa Mtwara; Bw. John Mwakipesile, aliyekuwa Mbeya. Wengine ni Kanali Enos Mfuru aliyekuwa Mara; Brig. Jen. Dk. Johanes Balele aliyekuwa Shinyanga; na Meja Jen. Mst. Said S. Kalembo aliyekuwa Tanga.

Wakuu wa Mikoa wanne waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni Bibi Amina Mrisho aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani; Dk. James Msekela aliyekuwa Dodoma; Bw. Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Bw. Daniel Ole Njoolay aliyekuwa Rukwa.

Wakuu wote wa Mikoa waliopo sasa wameagizwa kuandaa Hati za Makabidhiano (Handing Over Notes) katika muda wa siku 14 kuanzia siku ya kuapishwa kwa Wakuu wapya wa Mikoa. Aidha Wakuu wa Wilaya ambao wamepandishwa vyeo kuwa Wakuu wa Mikoa nao wanapaswa kufanya hivyo hivyo kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya watakaopangiwa vituo vitakavyokuwa vimeachwa wazi kutokana na uteuzi wao.

Wakuu wa Mikoa ile minne mipya na Wakuu wa Wilaya watakaoteuliwa hapo baadaye nao watatakiwa kuandaa Hati za Makabidhiano ndani ya siku 14 tangu kuapishwa.

Makabidhiano hayo lazima yahusishe pia kutembelea kwa pamoja baadhi ya maeneo na miradi ambayo ni muhimu kama sehemu ya makabidhiano yao.

Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa na Wakuu wa Mikoa minne mipya wakaoteuliwa pamoja na Wakuu wote wa Wilaya watakaoteuliwa baada ya zoezi kukamilika watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya wiki tatu kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kiuongozi na kiutendaji.

Wakuu hao wapya wa mikoa wataapishwa siku ya Ijumaa, Septemba 16, 2011 saa 4.00 asubuhi kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wakuu hao wapya wa mikoa; vituo wanavyokwenda na vituo walivyotoka ni kama ifuatavyo:

Na.JINA LA MKUU WA MKOAKITUO AENDAKOKITUO ATOKAKO
1.Bw. Saidi Mecki SadikiDAR ES SALAAMRC - Lindi
2.Bw. John Gabriel TupaMARADC - Dodoma
3.Bw. Saidi Thabit MwambunguRUVUMADC - Morogoro
4.Kanali Joseph SimbakaliaMTWARARC Kigoma
5.Bi. Chiku S. GallawaTANGADC - Temeke
6.Bw. Abbas KandoroMBEYARC Mwanza
7.Bw. Leonidas T. GamaKILIMANJARODC – Ilala
8.Dkt. Parseko Ole KoneSINGIDARC Singida
9.Eng. Stella ManyanyaRUKWAMbunge V/Maalum
10.Bibi Christine IshengomaIRINGARC Ruvuma
11.Dk. Rehema NchimbiDODOMADC - Newala
12.Bw. Elaston John MbwilloMANYARADC – Mtwara
13.Col. Fabian I. MassaweKAGERADC - Karagwe
14.Bibi. Mwantumu MahizaPWANIMbunge/NW Mstaafu
15.Bibi. Fatma A. MwassaTABORADC - Mvomero
16.Bw. Ali Nassoro RufungaLINDIDC - Manyoni
17.Eng. Ernest Welle NdikilloMWANZADC - Kilombero
18.Lt. Col. Issa MachibyaKIGOMARC Morogoro
19.Bw. Magesa S. MulongoARUSHADC - Bagamoyo
20.Bw. Joel Nkaya BenderaMOROGOROMbunge/NW Mstaafu
21.Bw. Ludovick MwananzilaSHINYANGAMbunge/NW Mstaafu



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM
JUMATANO, SEPTEMBA 14, 2011.

Wednesday, September 14, 2011

UNAFIKI WA CCM: Rostamu: Shetani-Malaika KWA WAKATI MMOJA????

Jina la Rostam ni jina maarufu sana masikioni mwa Mamilioni ya Watanzania - japo wengi wao ni kwa Ubaya, Chuki, hasira, Uchungu na....
Alijiuzuru Kutokana na Kuchoshwa na SIASA UCHWARA
ZA CCM.... LEO ANAWAOMBA KURA WANANCHI
WAKICHAGUE CHAMA CHENYE SIASA UCHWARA!!!!
Hivi karibuni, Muhasibu huyo mstaafu wa CCM Taifa, Kada wa Chama, Mjumbe wa Halmashauri ya CCM, NEC nakadhalika alikuwa Gumzo kubwa Ndani ya Chama hicho, kwenye vyombo vya habari na nchini kwa Ujumla kwamba YEYE ROSTAMU pamoja na wenzake Wawili NDIYO MAGAMBA ambayo Mwenyekiti wa Chama KIKWETE alikuwa anawaongelea kwenye maadhimisho ya Miaka 34 ya CCM mwezi Februari.


Baada ya hapo, Chama kilivunja Sekretariat na kuunda mpya ambayo ilianza kazi kwa Mbwembwe sana, kubwa ikiwa ni kutishia kuwavua "magamba" wa Chama hicho iwapo hawatajivua wenyewe ndani ya Siku 90! Baadaye ilikuja kufahamika kwamba ULIKUWA NI UONGO WA CCM kama kawaida ya Chama hicho! Siku 90 zilipita na hakuna kilichofanyika!


Siku kadhaa baadaye, Rostam Azizi, Mbunge wa Jimbo la Igunga (CCM) na kada mkuwa wa CCM aliamua kujiuzuru Ubunge na Siasa kwa sababu kubwa aliyoitaja kuwa ni SIASA UCHWARA za ndani ya CCM..!!! Aliposema CCM ina Siasa Uchwara, naamini alikuwa anamaanisha Kabisa kwamba KIKWETE, Mwenyekiti wa CCM ANA SIASA UCHWARA kwa maana Yeye ndiye Mwenyekiti na Kiongozi wa Chama hicho Chenye Siasa Uchwara!
Watu wanaofahamika wazi kuwa ni Mafisadi, Wanafiki,
Wasaliti wa Taifa hukemewa tu iwapo hakuna kampeni,
kampeni zikija huonekana ni wa Muhimu kwa Ushindi
na Hutumiwa "kurubuni" wapiga kura...
Mchakato wa kumpata Mrithi wa Rostam ulipoanza, nilishangaa kupata taarifa kuwa CCM Imepanga Kumtumia Rostam Azizi kufanya Kampeni ya Chama hicho Igunga!!!... Nilidhani utani kwa sababu ni UPUMBAVU ambao hata mtoto mdogo asingeweza kufikiria kwamba Chama "kikongwe" cha Siasa kama hicho kinaweza kuwa na maamuzi ya "kijinga" namna hiyo...


Rostam, ambaye Amesimangwa sana, amesemwa sana - kwa mafumbo na kwa wazi wazi na CCM... Rostam, aliyejiuzuru Ubunge kutokana na Siasa Uchwara za CCM, Leo ndiye anaongoza Kampeni za Kumpata Mrithi wake Kwa Idhini ya Chama hicho hicho chenye Siasa Uchwara?????


Kama Wananchi wakimsikiliza Rostam na Kumchagua Mbunge kutoka Chama Chenye Siasa Uchwara, nitajua Tatizo la Uchwara SIO LA CCM BALI LA WANANCHI..!!!


WANANCHI WAKICHAGUA MBUNGE KUTOKA KWENYE CHAMA CHENYE SIASA UCHWARA, NITAJUA ZAIDI KWAMBA TATIZO KUBWA LA HII NCHI SIO UCHWARA WA SIASA ZA CCM BALI UCHWARA WA AKILI ZA WATANZANIA!!!!

CCM Na Rushwa ya Wali IGUNGA!

Pasipo Sera Madhubuti zinazoambatana na Utekelezaji wake, Vyama vingi vitalazimika Kugawa Wali, Pilau, Mchuzi na hata Ugali ili kuweza kupata watu wengi kama hawa wa Kusikiliza Viongozi wake Wakihutubia.....


Jana wakati nikipekua katika kutafuta habari nilikutana na taarifa iliyodokeza kwamba CCM imeamua kutumia njia ya kugawa Wali na Mchuzi kwenye Mikutano yake ili kuvutia wasikilizaji na kununua wapiga kura kwa njia hiyo.


Nilipopata taarifa hiyo nikakumbuka maneno ya Tendwa John (Msajili wa Vyama vya Siasa) aliyoyatoa siku chache kabla ya Kampeni kuanza akionya Vyama (wakati ule akimaanisha vya upinzani) visitumie tatizo la Njaa Igunga kama njia ya Kugawia Rushwa ya Chakula - Mahindi na Unga - kwa Wananchi ili kuwanunua kwenye Uchaguzi!


Hatimaye nikafanikiwa kupata uthibitisho kwamba ni kweli Chama Cha Mapinduzi kimeamua kutumia njia hii ya "Kimapinduzi" kununua kura kwa Kugawa WALI-MCHUZI mkutanoni!
Wananchi Wakisubiri kula Wali kwenye Mkutano mmojawapo wa CCM huko Igunga. Kwa maeneo yenye njaa na hali ngumu ya kimaisha, Sahani moja tu ya wali inatosha sana kumnunua mpiga kura na akaiuza kura yake!


Taarifa hizi zikanikumbusha Siku chache zilizopita MBUNGE MMOJA WA CCM AALITHIBITISHIA KWAMBA YEYE ALISHINDA UCHAGUZI KWA NJIA ZISIZO ZA KIUCHAGUZI, katika jimbo  lake mojawapo huko huko Mkoani Tabora!


Pamoja na Ubovu wa Viongozi na Wanasiasa wetu, lakini UJINGA huu wa wananchi una nafasi kubwa zaidi katika kuendelea kuchelewesha maendeleo na kuongeza Ujinga, Ushenzi na Ubabaishaji miongoni mwa Viongozi wetu.


Wananchi Wanapewa Wali-Mchuzi, Wanaahidiwa Maendeleo halafu wanakaa kuyasubiri....


N.B: Pamoja na Kugawa WALI-MCHUZI, Picha inaonesha wengi waliohudhuria kumsikiliza Mzee Mkapa na CCM yake ni Watoto!!


N:B: HIKI CHAMA KUNA WAKATI KILIWAHI KUONGOZWA NA NYERERE!