Kumuhusu KIKWETE, ni taarifa kwamba alipewa "rushwa" na mmilikuwa wa Hoteli ya Kempiski - mwarabu Ali Albwardy. Kwa uelewa na uzoefu wa Viongozi wa Kiafrika, sikushangaa wala sikuona ajabu kwamba kitu kama hicho kinaweza kutokea....
Kiongozi wa kiafrika kupewa rushwa - nakuipokea kwa moyo mkunjufu - sio kitu cha ajabu - lakini hoja inarudi kwenye Rushwa yenyewe ni Nini?
Nchi nyingi za Kiafrika Zimeuzwa kwa Wageni tangu Kabla ya Ukoloni kwa Mikataba Mibovu ambayo kwa nyuma mingi huambatana RUSHWA |
Taarifa kwamba KIKWETE ALIPEWA RUSHWA YA SHOPPING, na Suti kama Tano hivi inazidi kumimina Chumvi kwenye vidonda vilivyojaa mioyoni mwa Watanzania! Watanzania wamekuwa na Kikwete kama rais wao kwa miaka kama Sita sasa na Ameonesha kwa Kiwango kikubwa sana KUSHINDWA kukabili Changamoto zinazolikabili.
KIKWETE AMESHINDWA kutoa suluhisho kwa Matatizo hata madogomadogo sana ambayo hata mtoto wa Sekondari akipewa mamlaka na madaraka ya kisheria na kikatiba aliyonayo Rais wa Tanzania angeweza kuyafanya!!!
Kiongozi aliyekaa madarakani kwa miaka 6 halafu mwaka wa Sita NDIPO ANAAHIDI kuwashughulikiwa waterndaji ndani ya serikali yake wanaokula Rushwa (wengi wao wakiwa ni wale aliowateua yeye mwenyewe); Hainishangazi hata kidogo kusikia AMEHONGWA NGUO!!!!!!
Viongozi wengi wanaouza nchi zao baada ya hapo hudharauliwa na kuonekana kama "wavulana" machoni pa "wanunuzi".... Madhara yake huwa ni mabaya zaidi kwa taifa zima |
Kitendo hiki kilichofanyika karne hii ya 21 kinaumiza zaidi pale kinaponikumbusha Historia tuliyofundishwa na Wazungu! Historia hiyo tuliyofundishwa inasema Wasukuma wa Shinyanga wali "uza" Almasi za mwadui kwa kubadilishana na Pipi walizopewa na Wazungu!!
Historia hii pamoja na kuniumiza, nilijitahidi kutokuiamini kwa sababu iliandikwa na Wazungu, hivyo nikadhani labda ililenga tu kudhalilisha utu wa mtu mweusi --- SASA NAYAONA MWENYEWE!!!
Kwa mtu aliyeko Mwadau mwaka 1880, ninaweza kumuelewa kwa urahisi sana kupokea Pipi na kutoa Almasi kuliko mtu anayeishi mwaka 2011, Mwenye Digrii ya Chuo Kikuu, Rais wa Nchi, Anayemiliki Ndege ya kifahari ya Ofisi yake - Kuhongwa Suti NA MWARABU!!!
Pamoja na kwamba haya yanaumiza na kudhalilisha taifa, mimi hayaniumizi sana kwa sababu Tangu Kikwete hajachaguliwa kuwa Rais mwaka 2005 niliwaambia Watanzania KIKWETE HAFAI KUWA RAIS WA NCHI...!!! Imani yangu haijabadilika, na inazidi kupata Uthibitisho wake...
Pole Tanzania, Pole Afrika kwa yanayokusibu.... Namuomba Mungu akuwezeshe eeh Tanzania na wewe Mama Afrika kuzaa Watoto watakaokuwa Tofauti na Hawa ulionao sasa hivi!!!
N.B: Sijui kama Kikwete alihongwa kweli hizo nguo, na hivyo sijasema alihongwa. Hoja yangu imejikita katika "tuhuma" hiyo, na sio ukweli au uongo wake...
No comments:
Post a Comment