Wednesday, September 14, 2011

CCM Na Rushwa ya Wali IGUNGA!

Pasipo Sera Madhubuti zinazoambatana na Utekelezaji wake, Vyama vingi vitalazimika Kugawa Wali, Pilau, Mchuzi na hata Ugali ili kuweza kupata watu wengi kama hawa wa Kusikiliza Viongozi wake Wakihutubia.....


Jana wakati nikipekua katika kutafuta habari nilikutana na taarifa iliyodokeza kwamba CCM imeamua kutumia njia ya kugawa Wali na Mchuzi kwenye Mikutano yake ili kuvutia wasikilizaji na kununua wapiga kura kwa njia hiyo.


Nilipopata taarifa hiyo nikakumbuka maneno ya Tendwa John (Msajili wa Vyama vya Siasa) aliyoyatoa siku chache kabla ya Kampeni kuanza akionya Vyama (wakati ule akimaanisha vya upinzani) visitumie tatizo la Njaa Igunga kama njia ya Kugawia Rushwa ya Chakula - Mahindi na Unga - kwa Wananchi ili kuwanunua kwenye Uchaguzi!


Hatimaye nikafanikiwa kupata uthibitisho kwamba ni kweli Chama Cha Mapinduzi kimeamua kutumia njia hii ya "Kimapinduzi" kununua kura kwa Kugawa WALI-MCHUZI mkutanoni!
Wananchi Wakisubiri kula Wali kwenye Mkutano mmojawapo wa CCM huko Igunga. Kwa maeneo yenye njaa na hali ngumu ya kimaisha, Sahani moja tu ya wali inatosha sana kumnunua mpiga kura na akaiuza kura yake!


Taarifa hizi zikanikumbusha Siku chache zilizopita MBUNGE MMOJA WA CCM AALITHIBITISHIA KWAMBA YEYE ALISHINDA UCHAGUZI KWA NJIA ZISIZO ZA KIUCHAGUZI, katika jimbo  lake mojawapo huko huko Mkoani Tabora!


Pamoja na Ubovu wa Viongozi na Wanasiasa wetu, lakini UJINGA huu wa wananchi una nafasi kubwa zaidi katika kuendelea kuchelewesha maendeleo na kuongeza Ujinga, Ushenzi na Ubabaishaji miongoni mwa Viongozi wetu.


Wananchi Wanapewa Wali-Mchuzi, Wanaahidiwa Maendeleo halafu wanakaa kuyasubiri....


N.B: Pamoja na Kugawa WALI-MCHUZI, Picha inaonesha wengi waliohudhuria kumsikiliza Mzee Mkapa na CCM yake ni Watoto!!


N:B: HIKI CHAMA KUNA WAKATI KILIWAHI KUONGOZWA NA NYERERE!

1 comment:

  1. KWELI WALICHOSEMA WAHENGA SASA KIMETIMIA!!!ULE USEMI WA MFA MAJI HAISHI KUTAPA TAPA!!NDO UMEWAKUTA NINYI WANA CHADEMA!! HAMUWEZI ENDESHA KAMPENI KWA AMANI PASIPO KUKASHIFIANA KIIVYO?INAMAANISHA WANANCHI WAIGUNGA NIWALOHO KIIVYO? MBONA NINYI MNATUMWAGIA TINDIKALI HATUSEMI?

    ReplyDelete