Alijiuzuru Kutokana na Kuchoshwa na SIASA UCHWARA ZA CCM.... LEO ANAWAOMBA KURA WANANCHI WAKICHAGUE CHAMA CHENYE SIASA UCHWARA!!!! |
Baada ya hapo, Chama kilivunja Sekretariat na kuunda mpya ambayo ilianza kazi kwa Mbwembwe sana, kubwa ikiwa ni kutishia kuwavua "magamba" wa Chama hicho iwapo hawatajivua wenyewe ndani ya Siku 90! Baadaye ilikuja kufahamika kwamba ULIKUWA NI UONGO WA CCM kama kawaida ya Chama hicho! Siku 90 zilipita na hakuna kilichofanyika!
Siku kadhaa baadaye, Rostam Azizi, Mbunge wa Jimbo la Igunga (CCM) na kada mkuwa wa CCM aliamua kujiuzuru Ubunge na Siasa kwa sababu kubwa aliyoitaja kuwa ni SIASA UCHWARA za ndani ya CCM..!!! Aliposema CCM ina Siasa Uchwara, naamini alikuwa anamaanisha Kabisa kwamba KIKWETE, Mwenyekiti wa CCM ANA SIASA UCHWARA kwa maana Yeye ndiye Mwenyekiti na Kiongozi wa Chama hicho Chenye Siasa Uchwara!
Watu wanaofahamika wazi kuwa ni Mafisadi, Wanafiki, Wasaliti wa Taifa hukemewa tu iwapo hakuna kampeni, kampeni zikija huonekana ni wa Muhimu kwa Ushindi na Hutumiwa "kurubuni" wapiga kura... |
Rostam, ambaye Amesimangwa sana, amesemwa sana - kwa mafumbo na kwa wazi wazi na CCM... Rostam, aliyejiuzuru Ubunge kutokana na Siasa Uchwara za CCM, Leo ndiye anaongoza Kampeni za Kumpata Mrithi wake Kwa Idhini ya Chama hicho hicho chenye Siasa Uchwara?????
Kama Wananchi wakimsikiliza Rostam na Kumchagua Mbunge kutoka Chama Chenye Siasa Uchwara, nitajua Tatizo la Uchwara SIO LA CCM BALI LA WANANCHI..!!!
WANANCHI WAKICHAGUA MBUNGE KUTOKA KWENYE CHAMA CHENYE SIASA UCHWARA, NITAJUA ZAIDI KWAMBA TATIZO KUBWA LA HII NCHI SIO UCHWARA WA SIASA ZA CCM BALI UCHWARA WA AKILI ZA WATANZANIA!!!!
huu ndio undumakuwili wa CCM,Siku zote wamekuwa hivyo,wanatenda kinyume na wanavyoongea,
ReplyDeleteushenzi mtupu
ReplyDeletepamoja ndugu yangu lakini ingefaa haya yakawafikia wana igunga.
ReplyDelete