Tuesday, January 10, 2012

MAUAJI Nigeria: TANZANIA Tunajifunza Nini?

Majimbo ya Kaskazini ya nigeria yanayotawaliwa
kwa kufuata Sharia (ya kijani) na ya kusini hutawaliwa
pasipo misingi ya kidini


Hivi sasa nchini Nigeria kuna mauaji ya kikatili yyanayoendelea kufanywa na kikundi cha Waislam, cha Kigaidi, kiitwacho Boko Haram. Kikundi hiki kilianzishwa Mohammed Yusuf (aliuawa July 2009 na majeshi ya Serikali) na hadi sasa kinapigania kutaka Nigeria yote kuwa ni taifa la Kiislam na linaloendeshwa kwa "Sharia". Jina Boko Haram ni la ki-Hausa likimaanisha "Elimu ya Ki-Magharibi ni Haram". Raman hiyo hapo juu inaonesha Majimbo ya Nigeria yanayotawaliwa kwa Sheria za Kiislam "Sharia".

Ghasia zinazoendelea Nigeria kwa sasa, pamoja na mambo mengine zimechangiwa na mambo yafuatayo:

1. Mgawanyiko wa kidini kati ya Kusini na Kaskazini mwa nchi (kusini wakristo na Kaskazini Waislam). Waislamu wengi sana wanaishi kaskazini - kama inavyooeshwa kwenye hiyo ramani hapo juu - na Wakristo wengi wanaishi kusini. Katikati ya Nchi ndipo makutanio ya dini hizi mbili - ambapo ndipo vurugu nyingi zinatokea.

2. Tofauti za kimaendeleo na kielimu (Wakristo wa Kusini wamesoma sana na wana maendeleo makubwa kielimu na kiuchumi ukilinganisha na Waislamu wa kaskazini ambao wengi hawajasoma (wamachukuliwa kama wajinga) na ni maskini).

3. Rais Goodluck Jonathan kuwa Rais kwenye awamu hii wakati Waislamu walikuwa wanadai ni Zamu ya Rais Muislamu (Chama tawala huwa kina utaratibu wa kugawanya zamu za Uongozi kwa kufuata dini - Wakristo kwa Waislam). Utakumbuka kuwa Goodluck alishika uraia kama miaka miwili iliyopita baada ya aliyekuwa rais wakati huo kufariki kabla ya muda wake kuisha. Kiutaratibu, zamu hii ilipaswa kuwa ya rais Mkristo (kama ilivyo sasa) lakini Waislamu walipinga asigombee urais kwa sababu wanadai alishakuwa rais tayari (kwa kuwa alishika nafasi ya aliyefariki - yeye alikataa).

Jambo hili liliwafanya Waislamu wengi hata katika chama tawala kukataa kumuunga mkono na kumuunga mkono mgombea wa upinzani ambaye alikuwa Muislamu (ambaye hata hivyo hakushinda).

4. Harakati za Waislamu kutaka Nigeria iwe taifa la Kiislamu na itawaliwe kwa kufuata "Sharia", jambo ambalo halikubaliwi na watu walio wengi - ikiwa ni pamoja na Wakristo, Wanajadi na Waislam wanaopenda kutenganishwa kwa Serikali na Imani za kidini....

Kwa kujua kuwa jambo hilo haliwezi kukubalika katika majimbo ya kusini, Waislamu hao kwa kutumia kundi lao la kigaidi (Boko Haram) lenye makundi matatu ndani yake yaliyotengana, waliamua kutumia njia ya vitisho, mauaji na ukatili mwingine ili kulazimisha matakwa yao ya utawala wa kiislamu katika taifa zima.
Mohammed Yusu (39),mwanzilishi wa Boko Haram,
 alikamatwa na Jeshi na
Kuuawa Mikononi mwa Polisi July 2009
 5. Harakati za Makundi ya Kiislamu yenye itikadi katika nchi mbalimbali duniani ambayo yana ndoto ya kuona nchi nyingi zaidi zikiwa za kiislamu na kutawaliwa kwa kufuata Uislam....

Huu ni upepo unaozidi kupuliza duniani kote na katika mataifa mengi ambako makundi mengi ya Waislamu hususan ya kigaidi (yanayotumia njia za mauaji ya kikatili ya raia na watu wasi na hatia) yanaendeleza harakati za kutaka mataifa husika yawe ya kiislamu na yatawaliwe kwa kufuata "Sharia"

6. Uchanganyaji wa Dini na Siasa. Baadhi ya wanasiasa nchini Nigeria walipoona kuna mgwanyiko mkubwa wa kidini katika jamii waliamua kutumia mgongo wa dini zao kama daraja la kupanda kisiasa.

Matokeo yake walichochea chuki na uhasama wa kidini ambao kwa sasa ndio unazidi kuligawa taifa. Chuki kubwa iliyojengwa na inayoendelea kushamiri nchini Nigeria ni matokeo - kwa kiasi kikubwa - cha siasa zinazojikita katika dini - makanisani na misikitini - badala ya kujikita katika masuala yanayowakabili watu wote kwa ujumla wao - bila kujali dini zao.


Tunajifunza nini Tanzania:

1. Sio vizuri kupuuza harakati zenye kuchochea Chuki, Uhasama na Utengano wa Kidini pale zinapokuwa ndogondogo maana zikikua madhara yake huwa ni makubwa sana..... Kundi la Boko-Al-Haram lilipoanza miaka ya 90 mwishoni hadi mwaka 2001/2002 lilipoanzishwa rasmi, Serikali ilidharau sana uwezekano wa kundi hilo kuja kuwa kubwa na kuleta madhara makubwa katika Taifa kama ilivyo leo.

2. Ujinga unapozidi katika jamii ni kitu cha hatari sana, maana watu wajinga huwa wakipata mtu wa kuwaunganisha na kuwachochea kufanya lolote wanaweza kulifanya. Muda mwingi sana jamii ya Waislamu wa kaskazini ya Nigeria walichukuliwa kuwa ni wajinga kwa sababu hawajasoma na hivyo wakaonekana kama watu ambao hawana na hawatakuwa na IMPACT yoyote katika jamii iliyojaa wasomi na Matajiri.

3. Uchanganyaji au utumiaji wa Dini katika Siasa ni jambo la hatari sana. Wanasiasa wengi hupenda kutumia Dini na makundi ya kidini kwa ajili ya kujipatia nafasi za uongozi kupitia uchaguzi, lakini madhara yake ni mabaya.

4. Tutie msisitizo sana katika kuielimisha jamii na makundi mbalimbali pasipo kujali dini au makabila, maana madhara ya kuwa na jamii ya watu wasioelimika na wanaojiona wametengwa ni makubwa sana...

Katika makala inayofuata, nitaangazia zaidi historia ya Boko Haram, kuanzishwa  na kukua kwake, mustakabali wake huko Nigeria na Mitazamo mingine ya Kiislamu katika mataifa mengine na namna ambavyo inaweza kukua, kubadilika na kuwa kama Boko Haram....

1 comment:

  1. yapaswa suala hili lifanyiwe mjadala wa kitaifa ili interests za makundi mbalimbali ya kijamii zisikilizwe na zisipuuzwe, pia elimu juu ya religious torelance pamoja umuhimu wa kushirikishana/kualikana ktk masuala mbalimbali kama sherehe za kidini na mengine pamoja na kuwalimit wanasiasa kutumia udini vipewe kipaumbele.

    ReplyDelete