Juzi wakati nimewasili tu kutoka katika mizunguko yangu kusini mwa Afrika nilikutana na Gazeti moja likuwa na kichwa cha Habari kisemacho KIKWETE KIGEUGEU! Wakati nikiwa bado natafakari uzito wa maneno kusemewa kiongozi wa Nchi na yeye akayasoma na watu wanaomzunguka wakayasona na kumuonesha kwamba anasemwa hivyo wazi wazi, jana nikakutana na lingine lenye kichwa cha habari IKULU INAPWAYA!
Kunishtua na kunishangaza kwa maneno haya hakukutokana na uongo wake au upya/ugeni wake katika fikra zangu (kwa maana MIMI BINAFSI naamini kwamba ni ya Kweli kabisa). Mshituko wangu ulikuwa katika hatua ambayo Tanzania imefikia kwa sasa.
Tumeizoea Tanzania inayoongozwa na Rais mtendaji, ambaye anajitahidi kuonesha busara, ufahamu, ujuzi, dira na upeo wake yeye binafsi katika kushughulikia matatizo yanayoibuka na kulikabili taifa. Jitihada za marais hao tuliowazoea zilifanya watanzania wengi kuamini kuwa Matatizo waliyonayo yataisha kwa maana Rais wao yumo anayashughulikia.
Imani hii ya wananchi kwamba WANA RAIS IKULU ambaye anashughulikia matatizo na changamoto zinazolikabili taifa (hata kama hafanyi hivyo), ziliwafanya wananchi wengi kumshangaa, kumkemea na hata kumpinga wazi wazi mtu yeyote aliyekuwa akijitokeza na kutoa Kauli zinazoonesha kumsanifu, kumkejeli, kumdharau au kutokutambua jitihada zinazofanywa na Rais wa Nchi katika kushughulikia matatizo yao.
Miaka michache iliyopita (namaanisha KABLA YA KIKWETE hajaingia madarakani), kauli yoyote iliyokuwa inatolewa na mtu, taasisi au chombo cha habari KUMUHUSU RAIS WA NCHI ilikuwa inajadiliwa sana, kuchambuliwa na wakati mwingine kupingwa na kulaaniwa hadharani kwamba ni ya kichochezi, ni yenye kudharau mamlaka au kubeza jitihada za kiongozi.
KIKWETE analaumiwa kwa mambo mengi, sio tu kwa Kutokuamua pale anapotakiwa Kuamua, bali hata kwa maamuzi MABOVU. ETI Chenge naye aliwahi kupewa Uwaziri na Kikwete!!! |
HALI HAIKO HIVYO TENA!
Tangu ndugu yangu huyu ameingia madarakani kwa mbwembwe na kishindo, MAMBO YAMEBADILIKA SANA. Sidhani kama kuna Mtanzania yeyote mwenye akili timamu leo ambaye anaiheshimu Ikulu kwa heshima ile ya enzi za Mwalimu wa kwanza (acha mwalimu wa Pili) au basi hata enzi za Mwandishi wa Habari BM.
Moja ya Watanzania (sina hakika kama ni Mtanzania anyway) waliowahi kuwa na tuhuma nyingi sana za UFISADI NA UOZO wa kisiasa ni Rostam. KIKWETE ALISHINDWA KUSEMA AU KUFANYA LOLOTE DHIDI YAKE! |
Kupwaya, katika matumizi ya kawaida, huwa ni ile hali ya kuingiza kitu kimoja katika kitu kingine na baadaye kubaini kwamba kile kilichoingizwa ni kidogo ukilinganisha na saizi ya kile kinachopokea! Kuna mifano mingi sana ambayo inaweza kutumika kuelezea upwayaji wa kitu fulani, lakini mfano rahisi zaidi ni ule wa mguu na kiatu! Pale WATU WANAPOSEMA KIATU KINAPWAYA, HAWAMAANISHI KWAMBA KIATU NI KIKUBWA BALI HUMAANISHA MGUU NI MDOGO!
IKULU INAPWAYA
Tangu kuingia kwa Kikwete katika Ikulu ya Tanzania na kutangazwa kuwa Rais wa Tanzania, kuna mambo mengi sana ambayo yamejitokeza yakimuhusisha yeye au watendaji walioteuliwa na yeye ambayo ukiyachunguza Hata kwa akili ndogo sana, utabaini kuwa kuna Pengo kubwa sana katika Ikulu ya Tanzania. Mambo mengi alyoyaamua, aliyoyafanya, ambayo hakuyaamua na ambayo hakuyafanya Kikwete, kwa ujumla wake yanaonesha kuwa kuna kitu kikubwa sana kinapingua Ikulu!
KIKWETE analaumiwa kwa tabia yake ya Kupenda kuzunguka Duniani na kusifiwa na Viongozi wa Mataifa tajiri wakati hali ya kimaisha ya Watanzania inaendelea kuwa mbaya |
Anapokutana na Kusalimiana na WAZUNGU huonekana kama alikuwa haamini kama kuna atakuja kushikwa mkono na Mtu Mkubwa kama huyo! |
Upungufu ambao unaambatana kwa kiasi kikubwa na HOFU ya kufanya maamuzi, kufanya maamuzi MABOVU, kutokuchukua hatua pale inapotakiwa, kuonesha kwa maneno na kwa matendo kwamba kuna Woga n.k. ni mambo ambayo yamewashawishi Watanzania wengi zaidi kuamini kuwa IKULU YETU INAPWAYA – TENA SANA!
Ndio maana katika Tanzania ya Leo, mtu kusema au kuandika waziwazi katika Gazeti kwamba RAIS WA NCHI NI KIGEUGEU, IKULU INAPWAYA n.k sio jambo linalohitaji kujadiliwa wala kukosolewa tena. Hata wale waliokuwa “waumini” wakubwa wa Serikali, ambao walikuwa tayari kuitetea Serikali ya nchi kwa gharama yoyote (ya maneno na majibizano), siku hizi WAMEJAWA AIBU na hawaoni kama kitu chochote cha kutetea katika Serikali na Ikulu yetu!
Mimi ningekuwa karibu na KIKWETE NINGEMSHAURI AJIUZULU awaachie nafasi watanzania Wamchague Rais, na akikataa kujiuzuru MIMI NINDIYE NINGEJIUZULU! Kuna watu wengine kufanya nao kazi wanaweza kukuchafulia CV na hata kukuharibia hadhi yako katika jamii na taifa kwa ujumla!
KIKWETE, NAKUSHAURI UJIUZURU TUCHAGUE RAIS!!!!
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.... Hakuna mtu ambaye hukosea mambo yote, hata Kiwete kuna Mengine huyafanya kwa Usahihi.... Nakuachia Msomaji unitajie ni yapi anayoyfanya kwa usahihi |
wasaalam....
No comments:
Post a Comment