Taarifa zisizo Rasimi nilizozipata kwa kufuatilia mijadala mbalimbali (ikiwemo kutoka kutoka kwa mtu mmoja anayeonesha kuwa ni Mfanyakazi wa Wizara hiyo) zinasema kuwa Wafanyakazi wa Wizara hiyo walilipwa Posho kwa kuhudhurisha "hafla" ya Kumpokea Katibu huyo "KIPENZI" hapo wizarani....!!!
Hii Hapa ni nakala ya Barua aliyoisaini Jairo akiagiza Idara zilizo chini ya Wizara yake kuchangia ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MOJA kwa ajili ya "kufanikisha" upitishwaji wa bajeti Dodoma! Chini ni Picha ya Jairo aliporejea Ofisini!
Hii ni nakala ya barua iliyosababisha Jairo kupewa "LIKIZO YENYE MALIPO" kwa tuhuma za jaribio la kuwahonga Wabunge |
"MAMA ZETU" Wakimpokea "kipenzi chao" Jairo kwa Shangwe nderemo na Vifijo Wakati aliporejea Ofisini..!!! |
Mdau mmoja alichangia hivi kuhusu huu Mjadala:
"JAIRO ...KWELI KAMANDA...WAKATI WA RICHMOND YEYE NDIYE ALIKUWA KATIBU WA WIZARA NA KAMATI YA MWAKYEMBE ALITAKA NA YEYE ACHUKULIWE HATUA...AKASAVAIVU.....H
UTETENZI WA CAG KUHUSU JAIRO
TUHUMA ZA JAIRO ILIKUWA NI KUKUSANYA BILIONI 1 KUTOKA KWA TASISI ZA SERIKALI ACCORDING TO BUNGE...LAKINI MCHUNGUZI WA CAG UMEONYESHA ALIKUSANYA MILIONI 500 NA SI BILIONI 1...KWA KUWA TUHUMA ZILIHUSU BILIONI 1 THEN JAIRO HANA HATIA....kwa kuwa wizara ina risiti ya matumizi ya hzo pesa
NIJUAVYO MIMI
hii sio issue ya CAG, kwa kuwa kazi ya CAG ni kuangalia kama matumizi ya pesa walifanyika kwa manufaa ya serikali,na sio kuangalia uhalali wa risiti...hata kama umefoji risiti unaweza ukawatoka CAG....hii ni issue ya TAKUKURU na POLISI kwa kuwa kuna mazigira na rushwa...na kufoji risiti
matumizi ya pesa
kati ya milioni 500 chenji ni milioni 123 ...huwenda zikatumika kumpongeza mzee kurudi kazini" Soma mchango huu wa Tumaini Thomas kwa Kubonyeza Hapa...
Unaweza kufuatilia mjadala mmojawapo unaohusiana na kurudi kwa Jairo Kazini na kupokelewa kwa Shangwe kwa Kubonyeza Hapa...
Wasaalam... mussa
No comments:
Post a Comment