Tuesday, August 9, 2011

KIKWETE Kupingwa kwa MAANDAMANO MAREKANI!

Nimepata Taarifa Hii Kwamba Watanzania Walio Marekani Wanajiandaa kufanya Maandamano ya Kupinga Safari Nyingine ya Kikwete huko Marekani (Nimeipata kupitia Wanabidii)


Tunaandaa maandamano ya amani jijini Washington DC Rais Kikwete atakapowasili kwenye kikao cha DICOTA 2011. Tayari watu 150 wamekubali kushiriki kwenye maandamano hayo. Tunataka watu wengi zaidi kujitokeza. Hii ni kumshinikiza huyu fisadi papa na mzururaji kushugulikia matatizo yanayowakabili wananchi wa kawaida. 


Maandamano yetu yatahitimishwa na kupokelewa na viongozikutoka United States Department. Tayari tumetuma maombi kupinga misaada marekani inayopa Tanzania, kwani hayasaidii Jamii bali Kikwete na genge lake la majambazi

Wote mnakaribishwa karibishwa. Maandamano ya Amani yanaruhusiwa marekani ilimradi mtu hajavunja sheria nchini. Ukiwa na makaratasi yako, njoo tulikomboe taifa letu. Ukombozi wa TANZANIA upo mikononi mwetu. Mabango yanachapishwa tarehe 24, Tunaomba mawazo tofauti kuhusu ujumbe tutakaobeba kwenye mabango yetu. 



Tumechoka na Kikwete, dawa nikuanza maandamano.Tupo tayari kufa sasa. Tunisia iliokolewa na watu tu kama sisi, tukifa bahati mbaya vizazi vijavyo vitafaidi. Tafadhali sambaza ujumbe. Tutatoa tamko rasmi ya maandalizi tarehe 20 mwenzi huu Ukitaka kushiriki tuma barua  pepe  EliakimMallya@yahoo.com

Raia wa kawaida anayo haki ya kumfanya Kikwete Anyimwe VISA. Kwa Kupinga Ujio wa Kikwete, au yeye kunyimwa VISA tumeni emails nyingi iwezekanavyo kwenda East African Affairs Bureau. Email Adress    wiegertjr@state.gov

No comments:

Post a Comment