Hii ni Nukuu ya Shy-Rose "Je unafahamu kwamba Rais JK ndiyo kiongozi anayechangia kwa kiasi kikubwa sana kukigawa hichi chama chetu?". Shy-Rose, ambaye katika siku za karibuni amejitokeza waziwazi na kuonesha kutoridhishwa na "performance" ya Kikwete kama Rais wa Nchi, amekuwa miongoni mwa Watanzania wachache ambao wamejitolea kuacha Unafiki na "Sifa za Kijinga" kwa kiongozi hata pale anapokosea.
Shy-Rose ameyasema maneno hayo kupitia mtandao wa Facebook alipokuwa akichangia "status" ya Chiligati iliyoandikwa "TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!!".
Pamoja na kauli hiyo nzito dhidi ya Mwenyekiti wa Chama tawala ambaye amekuwa akitajwa na wengi kuwa ameonesha kila dalili ya kushindwa kukiongoza chama hicho, Shy-Rose pia aliekemea tabia ya baadhi ya Wana CCM na wanachi kwa ujumla (hususan viongozi walio karibu na KIKWETE) kuwa wanamsifia-sifia Kikwete hata pale anapoharibu kazi. aliandika hivi "...wananchi wengi sana wameanza kukosa imani na CCM kutokana na fitna, majungu, unafiki wa kumsifia Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete, hata pale anapoharibu."
Maneno "mazito" kama haya wanapotamkiwa Viongozi wenye busara katika "nchi za watu" huwa wanajjibu kwa kujiuzuru ili kuwapisha viongozi wenye uwezo zaidi, sijajua Busara ya kiongozi wetu itamuongoza kufanya nini, kwa maana maneno kama haya ameshasemewa mara nyingi MNO, lakini ndo kwanza anaongeza safari za kwenda Marekani!
MUNGU ISAIDIE TANZANIA (maana ulishaibariki siku nyingi ila UPOFU "wetu" ndio unatufanya tuendelee kuomba "baraka").
Hapa Chini ni Maandishi ya Shy-Rose kutoka kwenye "Wall" ya John Chiligati:
"@Mhe. John Chiligati kauli mbiu kama hizi ndizo zinazoturudisha nyuma. Tazizo moja kwenye Serikali ya CCM tunaongoza kwa kauli mbiu lakini utekelezaji ndiyo kasheshe...huu siyo tena wakati wa mbwembwe za kauli mbiu, ila kikubwa kinachotakiwa ni utekelezaji. Mimi naomba nikwambie ukweli kuhusu mtazamo wa watanzania leo juu ya chama chetu CCM...wananchi wengi sana wameanza kukosa imani na CCM kutokana na fitna, majungu, unafiki wa kumsifia Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete, hata pale anapoharibu. Ni ukweli usiopingika kwamba leo hii CCM iko katika hali mbaya kimtazamo mbele ya macho ya jamii. Je unalifahamu hili Mhe Chilligati? Je unafahamu kwamba wananchi wameanza kuichoka CCM? Je unafahamu kwamba Rais JK ndiyo kiongozi anayechangia kwa kiasi kikubwa sana kukigawa hichi chama chetu? hivi mnamwambia ukweli wa mambo au mnampotosha kwa kutomwambia ukweli? Nitashukuru sana ukimfikishia ujumbe wangu JK kwamba style yake ya uongozi ndani ya chama chetu na akiwa kama mkuu wa nchi inalalamikiwa sana huku mitaani, hata na mwananchi wa kawaida...kila mtu anauliza JK yuko wapi? mbona yuko kimya sana? Mwambie wananchi wanataka kuskia kauli yake nchi inapoelekea kwani kila kikicha kuna matatizo lukuki...kwa leo ni hayo tu Mhe. Chilligati...naomba kuwasilisha!
No comments:
Post a Comment