Friday, October 28, 2011

DOWANS: Kamanda KOVA Anasikitisha na Anashangaza!

Kamanda Wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam
Jana jioni nikiwa katika Shughuli zangu za Kijamii nilipokea Simu kutoka kwa Mhariri wa Gzeti moja la Kila siku la Kiingereza akiniuliza nilikuwa na Mtazamo gani kuhusiana na Kauli ya Kova Kusitisha maandamano ya Kupinga kulipwa kwa DOWANS siku ya Jumamosi, nilipigwa na butwaa lakini nikamwambia tu Ampigie Simu Mwanasheria Wetu atampa maelezo kamili.


SIASA ZA DOWANS
Wakati akisoma Hukumu iliyoagiza TANESCO wailipe DOWANS, Jaji Mushi wa Mahakama Kuu alisema "Nafahamu fika kuwa kesi hii ya Dowans ina sayansi nyingi sana za kisiasa".


Ni jambo lililo wazi na linalofahamika kwamba kuna  nguvu kubwa ya kisiasa inayolizunguka suala la DOWANS, hivyo ni muhimu kuangalia na kuzingatia uwezekano wa kuwepo kwa "Siasa" katika maamuzi yoyote yanayofanywa kuhusiana na Suala hili.


"Visingizio" Vya Kova
Leo niliposoma kwenye Magazeti Kova alinukuliwa akitoa sababu kubwa ya kuzuia Maandamano hayo kuwa ni "Tishio la Mashambulizi ya Al-Shabaab".


Tuichambue Hiyo sababu
1. Kamanda Kova alipoulizwa kuhusu Mikusanyiko mingine ambayo na yenyewe inaweza ikashambuliwa na Al-Shabaab alisema ETI Al-Shabaab Wanapendelea Sehemu ambazo Zina Wanaharakati. Sipendi Kusema HUU NI UONGO lakini sidhani kama Kova mwenyewe ana uthibitisho wa kauli hii. Nitaichambua hapa Chini.


2. Pili, Alipoulizwa kuhusu Mechi ya Simba na Yanga ambayo na yenyewe itachezwa siku hiyo hiyo ambapo Yeye amekataza maandamano kwa sababu za Kiusalama akasema "Kutakuwa na Ulinzi Mkali". Suala la kujiuliza hapa, POLISI ishindwe kuhakikisha Usalama kwa waandamanaji 1,000 (Elfu Moja) POLISI hiyo hiyo ihakikishe Usalama wa watu 60,000 (Elfu Sitini) Uwanja wa Taifa?
Uwanja Wa Taifa Unachukua watu 60,000 mara 20 ya
Waandamani ambao Kova Alisema Hawataweza
kuwahakikishia Usalama!
Na zaidi ya hapo, POLISI Iko tayari kuwalinda na kuwahakikishia usalama Mashabiki wa Mechi ya Mpira wa Miguu LAKINI Polisi hao hao hawawezi kuwahakikishia usalama wananchi wanaoandamana kutimiza haki yao ya kikatiba NA KUTETEA MASLAHI YA TAIFA....


Madai ya Kova  ETI Al-Shabaab Wanapendelea Walipo Wanaharakati


Matukio ya hivi karibuni ambayo yalipelekea uwepo wa wasiwasi wa Mashambulizi ya Al-Shabaab hapa Nchini ni mashambulio ya Al-Shabaab yaliyofanywa huko Kenya. Mashambulio hayo yalikuwa kama Ifiatavyo:


Shambulio la Kwanza: Bomu la kutupwa kwa mkono lilirushwa kwenye kituo cha Matatu (Daladala) na kujeruhi watu kama 10 hivi


Shambulio la Pili: Bomu lilitupwa kwenye Night Club moja Nairobi na kuua Mtu Mmoja na Kujeruhi wengine kadhaa.


Shambulio la Tatu: Al-Shabaab walishambulia kwa maguruneti gari lililokuwa na Mitihani ya Shule na kumuua Afisa Elimu na mtu mwingine.


Kabla ya Hapo:
Kwanza, Alshabaab walimteka Nyara mwanamke mmoja Mtalii pwani ya Kenya na kumuua mumewe kwa kumpiga Risasi


Pili: Waliteka wafanyakazi wa Shirika la Medicins Sans Frontier (madaktari wasio na Mipaka) huko Kasikazini mwa Kenya na Kutokomea nao Somalia (Tukio hili lilifuatiwa na jeshi la Kenya Kuingia Somalia na Kuanza Vita Rasmi na Al-Shabaab)!!


MAPENGO Hotuba ya Kova!
Katika matukio hayo yote, hatuoni eneo hata moja ambapo Al-Shabaab wanawalenga wanaharakati...!!!!! Maelezo ya Kova yametokana na MSINGI UPI????? Wanaharakati wapi waliowahi kushambuliwa na Al-Shabaab??? 


Na zaidi ya hayo, KWANI ALSHABAAB WANAFUNGAMANO NA DOWANS hadi wawakasirikie Wanaoipinga DOWANS????


Tafakari yangu hadi hapo ilinirudisha nyuma kwenye Maneno ya Jaji Mushi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam: "Nafahamu fika kuwa kesi hii ya Dowans ina sayansi nyingi sana za kisiasa"....


Hoja za Kova nimezitafakari na kweli, kwa kiasi kikubwa sana ZINAPWAYA. Ni nyepesi mno kuweza kutolewa kama kisingizio cha kuzuia Maandamano ya Kudai haki na kutetea Raia wa Tanzania na mali zao!


Kama hoja na Sababu ni hizo tu, basi Kova amenisikitisha sana, maana sikutarajia kama Mtu mwenye nafasi ya juu kama yake kutoa hoja nyepesi kiasi hicho kupinga jambo zito kiasi hicho --- Lakini, Iwapo kuna sababu za kisiasa ambazo hakuzitaja - basi namuelewa!


Nina Imani siku moja Tanzania tunayoitaka Itapatikana, lakini kuna dalili za Wazi kwamba Bado Safari ni Ndefu na Ina mashimo na Miiba Mingi...


Wasaalam, ...//msb

7 comments:

  1. Poleni wanaharakati, Naamini ipo siku haya yote yatapita nimeguswa na kuumizwa na taarifa ya kusitisha maandamano haya, sijui mwisho wa haya ni lini? ila hakuna marefu yasiyikuwa na ncha.Ipo siku tutafika kwenye ncha na ndipo tutajua mbivu na mbichi.
    Renee

    ReplyDelete
  2. Twendeni barabarani tuache uwoga!

    ReplyDelete
  3. sijapata kuona watu wa ajabu namna hii haki ya MUNGU.Maswala muhimu ya taifa hili na wananchi wake wote pamoja na kova wanayawekea mizengwe utadhani wako katika hizo nyadhifa kwa bahati mbaya? pole Tanzania na watanzania wote

    ReplyDelete
  4. wanashindwa kulinda shilingi yetu,inaporomoka kila siku,mafisadi wanaongezeka kila siku hata hawa wenyeviti wa serikali za mitaan ni mafisadi sana,mfano kuna m/kiti mmoja huku mbezi juu anauza maji,kwa kuteka maji yote mchina aliyosambaza kwa ajili ya watu wengi,sasa anatumia mtu mmoja bwana londa.

    ReplyDelete
  5. Siku zote Kova hajawahi kuwa logic katika statements zake zote. Ni mtu anayetumwa kwenda kusema pasipo kufkiria maswali yanayotokana na taarifa yake ndiyo maana alipoulizwa sababu za msingi, alitoa majibu yasiyokuwa na mashiko. Ina eleweka, yupoyupo tuu kisiasa na si kiweledi. Anasema bila kufikiri athari ya maneno yake.

    ReplyDelete
  6. Binafsi pia huwa ananisikitisha sana.... statement zake nyingi huwa zinaacha maswali mengi HATA KWA MTOTO MDOGO wakati yeye nadhani akiamini kuwa atasikilizwa na kuaminiwa kwa sabau ya cheo na nafasi yake..... poor!

    ReplyDelete
  7. Askari Polisi nao wamekuwa wanasiasa?

    ReplyDelete