Thursday, October 13, 2011

MDAHALO NA RAIS: Jumatatu, Tar. 17 October!

Kampeni ya Ondoa Umaskini Tanzania - ambayo ni muunganiko wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali Tanzania yanayojishughulisha na Kupambana na Umaskini yameandaa Mdahalo maalumu siku ya Maadhimisho ya Siku ya Umaskini Duniani - Jumatatu tarehe 17 October 2011.


Mdahalo huo ambao umepangwa kuhusisha Asasi za Kiraia na wananchi kwa Ujumla kwa Upande Mmoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Pili, Utafanyika katika Ukumbi wa Waterfront, Dar es Salaam.


Taarifa zilizopatikana hivi karibuni kutoka Ikulu, hata hivyo, zimesema kuwa Rais Jakaya Kikwete hataweza kuwepo kwenye Mdahalo huo kwa sababu atakuwa kwenye safari ya kikazi. Kwa sababu hiyo, Makamu wa Rais, Dr. Gharib M. Bilal atahudhuria mdahalo huo.


Mdahalo huo ambao utafanyika kuanzia saa Nne Asubuhi hadi saa Sita Mchana, uko wazi kwa Viongozi na Watendaji katika Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Umma kwa ujumla. HATA HIVYO, mtu YEYOTE mwenye nia ya kuhudhia mkutano huo atatakiwa kutoa Taarifa ya Nia yake ya kushiriki kwa Afisa Mratibu wa Mkutano huo kupia email: m.billegeya@tango.or.tz na atapewa majibu iwapo nafasi bado zipo hivyo aweze kuhudhuria.


Mada mbalimbali zitawasilishwa siku hiyo na Wawakilishi wa Asasi Mbalimbali za Kiraia kuhusiana na Masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uwajibikaji, Madini, Rushwa, haki za Binadamu, Jinsia, Elimu n.k.

No comments:

Post a Comment