Saturday, October 1, 2011

UGAIDI: Tanzania Hatuna Serikali!!!!!

Hivi Karibuni nilicheka na kuumia sana kwa wakati huo huo wakati nilipokuwa nikimuangalia Katibu mkuu wa Chama Changu CCM "Mzee" Mukama akiwaeleza Waandishi wa habari kwamba CHADEMA kimeingiza "magaidi" kutoka nje ya nchi kwa ajili ya Kuvuruga Uchaguzi wa Igunga!


Kilichonichekesha ni ujinga na ukosefu wa busara au hata upeo kidogo kwa kiongozi wa Chama tawala kuwatangazia Watanzania kwamba kuna Magaidi yameingia nchini hhadi yamefika Igunga bila kukamatwa wakati Serikali iliyopo Madarakani ni ya Chama Chake....!!! HUU ULIKUWA UPUMBAVU - HATA KAMA NI KWELI WALIKUWEPO HAO MAGAIDI!


Katibu Mwenzake wa CHADEMA alipoulizwa kuhusiana na suala hilo na TBC1 alisema iwapo ni kweli CHADEMA kimefanya hivyo, kuingiza Magaidi kutoka Libya na Pakistan hadi Igunga, na guest Walipo zikafahamika LAKINI HAWAKAMATWI - basi CHADEMA NI CHAMA MAKINI SANA na watanzani wana kila sababu ya kukiamini chenyewe na SIO CCM! Majibu haya nadhani ndiyo yalikuwa majibu sahihi kwa TUHUMA YA KIPUMBAVU KISIASA KAMA YA MUKAMA!


Niliumia kwa sababu sikuamini kwamba Chama Changu cha CCM, kilicho wahi kuongozwa na Nyerere KIMEFILISIKA NA KUCHAKAA KISIASA kiasi cha kuongozwa na mtu mwenye fikra duni na chakavu kisiasa kama Mukama!


Leo wakati nasoma Email nilipokea email kutoka kwa MBUNGE WA NZEGA, HAMIS KIGWANGALLA akisema kuwa kuna Vijana wa MUNGIKI ambao Wamekamatwa Igunga wakiwa kwenye Coaster 2 na wameletwa kutoka Kenya kwa ajili ya kusaidia chama fulani cha Siasa!


Nisingependa kuingia Ndani sana kujadili maana ya kauli hizo kutoka kwa viongozi waandamizi wa CHAMA TAWALA NA MAANA YAKE KISIASA, lakini nadhani ni wakati Watanzania wakaona ni kwa kiasi TANZANIA TUNA SERIKALI HOVYO KABISA!!!!!


Kauli hizi zinamaanisha ni aidha TUNA CHAMA TAWALA KIBOVU au WANACHAMA WAKE NDIO WAPUMBAVU...!! Nadhani kwa hawa wapumbavu wengi wa CCM wanaotoa hizi kauli wasichoelewa ni kwamba kauli hizi zote kwa pamoja zinalenga kuwaonesha Watanzania kwamba wako hatarini na kwamba TANZANIA HAKUNA SERIKALI INAYOWEZA KUWAHKIKISHIA USALAMA WATANZANIA...!!!


Kama Gaidi anaweza kuingia nchini hadi akafika Igunga - NA ASIKAMATWE, Mungiki wakatoka Kenya Kwa Coaster hadi Igunga na Wasikamatwe, basi Tanzania iko katika Hatari kubwa sana ya kushambuliwa na Magaidi, tena kama maelezo hayo ya wana CCM ni ya kweli, basi Tanzania HATUNA SERIKALI!!!


..nitarudi!

No comments:

Post a Comment