Thursday, May 24, 2012

Mbunge wa Rombo (CHADEMA), Selasini, Apata Ajali Mbaya!

Joseph Selasini
 Taarifa zilizopatikana jioni na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro zinasema kuwa Mbunge wa jimbo la Rombo, Joseph Selasini, amepata ajali mbaya ya gari eneo la Bomang'ombe, wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Ajali hiyo imetokea wakati gari alilokuwa akiliendesha kupasuka tairi la mbele na kupinduka eneo la darajani. Taarifa za awali zinasema kuwa watu WATATU kati ya Watano waliokuwemo kwenye gari hilo Wamefariki Dunia hapo hapo - akiwemo Mama yake Mzazi na Shangazi yake!
Anafahamu na Kiarabu pia...
Yeye mwenyewe pamoja na baba yake - ambaye taarifa zinasema kuwa alikuwa akitoka kumchukua kutoka hospitalini - wamejeruhiwa na wamelazwa katika Hospitali ya Hai - Kilimanjaro - na hali zao zinaendelea vizuri.

Taarifa za ajali hii pia zimethibitishwa na mbunge huyo kupitia ukurasa wa Mtandao wa Kijamii Facebook.

Muda Mfupi Kabla ya Ajali

Muda Mfupi kabla ya ajali Mh. Selasini aliandika katika Ukurasa wake wa Facebook taarifa inayoonesha kiasi cha Pesa ambazo amekwisha kuzitoa kwa vijiji na jamii ya jimboni kwake kwa ujumla tangu achaguliwe kubwa mbunge wa jimbo kwa tiketi ya CHADEMA ambayo kwa pamoja inazidi MILIONI 50...!!!
Taarifa hii aliitoa Muda Mfupi kabla ya Ajali
Blogu hii itakuleteeni taarifa zaidi kuhusiana na maendeleo ya Afya ya Mbunge huyo, baba yake pamoja na taratibu nyingine za msiba wa ndugu zake hao wengine waliofariki katika ajali hiyo.

Pigo kwa CHADEMA

Ajali hii imekuja siku ambayo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilikuwa katika Sherehe na shamra-shamra nchi nzima kufuatia Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam kumtangaza Mbunge wa Jimbo la Ubunge - John Mnyika - kuwa Mshindi katika kesi iliyokuwa inamkabili dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Mnyika akisherehekea Ushindi Mahakamani Mapema Leo

Mbunge mwingine wa CHADEMA, Regia Mtema, alifariki miezi kadhaa iliyopita kwa ajali ya gari akiwa njiani kutokea Dar es Salaam kuelekea Morogoro.
Ajali nyingine ya gari ilimuua Mbunge wa CHADEMA, Regia Mtema


3 comments:

  1. Kweli inahuzunisha na kushtua ila sijui kwanini waheshimiwa wetu wanapenda kuendesha wenyewe tena mida ya jioni. Inaonekana alikuwa anakwenda Rombo, na muda huo wa jioni ikizingatiwa barabara ya Rombo ni lami mpya na nzuri, lazima angeendesha kwa spidi. Haukuwa uamuzi mzuri kusafiri muda wa jioni ingawa bado alikuwa hajafika hata nusu ya safari. Umefika wakati waheshimiwa wetu wachukue tahadhari sana.

    ReplyDelete
  2. Nashindwa kusema chochote; kibinadamu pole, lakini kwa nini ukimbize gari wakati hufiki dakika tano!!!

    ReplyDelete
  3. Poleni kwa Ajali Pia Mungu awabariki majeru wapate naafuu na kupona haraka

    ReplyDelete