Nembo ya JUMIKI, Zanzibar |
Taarifa zilizotoka Zanzibar zimewashtua na kuwahuzunisha watu wengi - hususan kitendo cha Watu kuvamia Kanisa, Kulibomoa na Kulichoma moto - katika harakati zao za Kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar!
Kanisa lililochomwa Zanzibar |
Japo ni kweli kwamba kuna haja ya Suala la Muungano kuwekwa wazi machoni pa Watanzania wote, kujadiliwa hadharani na hatimaye kufanyiwa maamuzi ya wazi - lakini ni lazima tuelewe kwamba kwanza kuna njia sahihi za kuweza kufanya hivyo, na Pili na MUHIMU ZAIDI, tuwe makini na watu wanaotaka na wanaoweza kupenyeza Ajenda zao za Siri na za Uovu katika mchakato huo.
Ni ukweli usiopingika kwamba kanisa la TAG Tanzania halikuhusika katika kuuanzisha Muungano, sina uhakika kama lina sera ya kuuimarisha na au kuudumisha Muungano, lakini muhimu zaidi, halina sera ya kupinga kujadiliwa au kupigiwa kura ya maoni suala la Muungano. Suala la Kushambuliwa kwa kanisa hilo ni dalili ya wazi kwamba KUNA WATU WAOVU ZANZIBAR - wenye Dhamira na Malendo ya Kigaidi - ambao wanataka kutumia vurugu zinazoendelea Visiwani humo kutekeleza uovu wa kidini na kigaidi!
Zanzibar! |
Kushambuliwa kwa kanisa hili na watu wanaodhaniwa kuwa katika harakati za kudai Kura ya maoni kuhusu Muungano ni wazi kwamba harakati hizo zinaanza (kama sio kwamba tayari) zimekwisha kuingiliwa na WATU WAOVU, ambao wanataka kutumia mwanya wa kuwepo kwa vuguvugu na harakati hizi kutekeleza uovu wao ambao aidha uko katika misingi ya kidini tu au umechanganyikana na dhamira ya UGAIDI ndani yake!
Katibu wa JUMIKI - anatafutwa na Polisi Zanzibar! |
Napenda kutoa tahadhari hii kwa taifa letu hili kwamba tusifanye kosa la kufumbia macho uovu huu unaoanza kama vile unafanywa na makundi ya watu wahuni, maana madhara yake hakika yatakuja kuwa makubwa kupita tunavyoweza kufikiria kwa sasa.
Uzoefu wa Nigeria!
Nchini Nigeria, wakati kundi la Boko al Haram lilipoanzishwa mwishoni mwa miaka ya 90, lilidhaniwa na kuchukuliwa tu kama kundi la kidini la Waislam ambalo lilikuwa linapenda na kuhamasisha elimu ya kiislam. Lakini ukweli ni kwamba malengo ya kundi hilo tokea mwanzoni yalionesha dalili za wazi kuwa iwapo litaachwa na kuendelea kukua na kujipanua, litakuja kuwa kundi la hatari sana nchini humo.
Kiongozi wa BOKO Haram, Aliua wengi kabla hajauawa! |
Miaka 10 baadaye, ni kundi kubwa zaidi la Ugaidi nchini humo ambalo sio tu linataka kulazimisha watu wote kuwa Waislamu (KWA LAZIMA) bali linaitumia nafasi hiyo kufanya Vitendo vya Kishetani vya Mauaji ya Kikatili dhidi ya raia wa Wasio na hatia - Ambao linadai ndio linataka wawe Waislamu!
Mbaya zaidi - lifanya Ushetani na Uovu huo wote CHINI YA KIVULI CHA DINI - uislamu - jambo ambalo linakisaidia kikundi hicho kujipatia wafuasi wengi wa dini ya kiislamu ambao hudanganyika kwa kudhani linatetea maslahi yao (japo kwa njia ambazo sio za kidini kabisa)!
Shambulio la Boko Haram kwenye kanisa, Nigeria! |
Kikundi hiki kilichoanza kama vuguvugu la kutaka Nchi Nzima Nigeria iwe ya Kiislamu na kufuata Sharia, kwa sasa limejikita zaidi katika kushambulia Makanisa na kufanya mauaji ya wakristo kila linapopata nafasi ya kufanya hivyo. Kitendo hiki ni cha Kisenzi na Kishetani ambacho hakiungwi mkono na Dini yoyote - hata Uislamu wenyewe - ambao Waovu wanaohusika wanadai wanaupigania na kuueneza!
Wito wangu kwa taifa!
Wito wangu kwa taifa tangu sasa Serikali iwe ya kwanza kujitokeza hadharani na KULAANI kitendo hicho cha Zanzibar na kuwatafuta na kuwafikisha wahusika wote mbele ya Sheria - bila kujali Imani zao za Kidini au dhamira zao katika kufanya Uovu huo!
Kanisa la TAG, limechomwa moto Zanzibar |
LAKINI kwa upande mwingine, ni muhimu Serikali ikajifunza kusikiliza na kuelewa matakwa ya Umma na kukubali kuusikiliza umma na kufanyia kazi mawazo yao. Sio wakati wa Serikali kuendelea kudhani kwamba zitaendelea kuwatawala wananchi wake kama mabubu na mbumbumbu ambao wako tayari mara zote kunyamazishwa na Serikali na kuzuiliwa kuyazungumzia masuala ya nchi yao - ETI kwa sababu tu Serikali na au Chama kilichoko madarakani hakijisikii vizuri kulizungumzia suala husika!
Hii SIO Zinjibar, Yemen, NI Zanzibar, Tanzania! |
Serikali yetu isijidanganye kwamba Watanzania (wa bara na visiwani) wataendelea milele na milele kukaa kimya kuhusu Muungano. Jitihada za serikali kukwepa kuliweka suala la muungano huu tata hadharani ili ujadiliwe na kufanyiwa maamuzi na hazitadumu siku zote. Ukweli utabakia kwamba kukataa kuuzungumza Muungano kwa sasa SIO kuuimarisha BALI ni kuchelewesha kuvunjika kwake!
Mabomu na Risasi Haviwezi Kudumisha Muungano Siku Zote |
Mimi nashangaa sana ninapoona mtu amepanda mbegu halafu anaukataa mti ulioota kwa mbegu aliyopanda.Waislamu wa zanzibar kama walivyo wengine wote Tanzania wamefundishwa na wakahamasishwa kuwa adui wao ni Muungano na MFUMOKRISTO (REJEA TAMKO LA JUMIKI LA 31/10/2010 Ambalo lilikuwa na kichwa TAMKO LA WAISLAMU DHIDI YA WAKRISTO).Sasa wazanzibar wameelewa mafunsisho ya viongozi wao,wahadhiri wao na walezi wao wa kiroho kwa kutilia maanani kuwa JUMIKI na kikundi cha uamsho zanzibar ni vikundi vya dini ya kiislamu.Ninasikitishwa na namna wazanzibar wanavyosingiziwa uhuni,ugaidi na kila jina baya kwa kutekeleza kwa usahihi mafunzo ya waalimu wao.Hii ni kuwatukana wazanzibar kuwa hawana uwezo wa kufikiri ama kutenda kama watu makini.Inasikitisha zaidi kuona kuwa anayewakashifu hivi ni yule yule aliyewafundisha na kuwahamasisha. Tujaribu kuliangalia jambo hili katika mazingira ya wakati wa fujo zile.Wazanzibar wamehamasishwa kuandamana kwa amani kupinga muungano.Wamekubali na kuhamasika kufanya maandamano haya kwa sababu wamekubali na kuamini kile ambacho viongozi wa kikundi cha uamsho wamekuwa wakiwaelimisha karibu miezi mitatu hivi.Wanapita mtaa wa kwanza,wa pili na labda mtaa wa tatu.Kisha polisi ambao kwa mafundisho ya JUMIKI na hata wana uamsho wazanzibar wanaona kuwa wanatekeleza amri za MAASKOFU ambao ni viongozi wa kikristo wanatokea,wanamkamata kiongozi wa waislamu wa zanzibar kutoka kikundi cha uamsho.Waandamanaji ambao ni wafuasi wa kiongozi huyu wanataharuki.Kiongozi wao amekamatwa na polisi,vibaraka wa MAASKOFU.Wanashikwa na ghadhabu,wanasahau kuwa wapo zanzibar,wakiwa na ndugu wakristo na wengine waislamu,kwamba ndugu zao wengine zanzibar wanaishi na wakristo tanzania bara.Wanaamua kudhihirisha hasira zao kwa vibaraka hawa wa maaskofu.Mawe yanarushwa,mabomu ya machozi yanarushwa,kisha jambo moja linaongezeka.Magari yanachomwa,kisha makanisa yanachomwa,bara bara zinafungwa kwa mawe,matairi ya magari yanachomwa.Habari zinasambaa kama nyasi kuwa zanzibar hali si shwari,kuna machafuko,tena kesho yake magazeti yanatoa taarifa ya kinachoendelea.Baada ya siku moja waalimu na viongozi wanatoa tamko kuwa waliofanya vurugu zile ni wahuni.Baadaye waalimu hawa wanakuja na matamko yasiyo rasmi kuwa kuna mapandikizi wanaoionea gele serikali ya umoja wa kitaifa ya zanzibar,halafu kiongozi wa uamsho anaendelea kukana kabisa kuwa taasisi yake haihusiki.Baadaye MAASKOFU WANATOA MATAMKO YAO.KISHA MAGAZETI YA AL NUUR YANAWAJIBU MAASKOFU KWA KEJELI.Hivi ni kwa nini hatupendi kusema ukweli???? Tunakwepa nini kusema ukweli??? Waislamu wametoa tamko linalotaka nchi igawanywe kwa kufuata wingi wa watu wenye dini fulani ili iwe nafuu kwa waislamu kuweka Mahakama ya kadhi na kujiunga na OIC.Wazanzibar wanaona kuwa wakiwa na nchi yao umasikini uliopo utaisha.Wahadhiri wa dini ya kiislamu wamebeba wajibu wa kuwafungua waislamu na kwa hakika wamefanikiwa sana kwa eneo la Zanzibar na hata bara kwenye mikoa waliyokwisha pita uelewa wa waislamu juu ya kinachoitwa dhuluma za KANISA ni mkubwa sana.Ni wakati sasa wa waislamu kama mlivyotoa tamko lile la tarehe 30/10/2010 kusimamia agenda zenu badala ya kuzipiga chenga kwa kujibingirisha na mambo ambayo si msimamo wengu.Kinyume chake wahadhiri kwa kiislamu wawaombe radhi waislamu kwa kuwafundisha kitu ambacho si msimamo wao.Wawaombe radhi wazanzibar kwa kuwagombanisha na wakristo ambao wameishi nao kwa miaka nenda rudi bila kufarakana nao. Hii itakuwa namna halisi ya kutatua matatizo na OMBWE LINALOTUKIA SASA.
ReplyDelete