Wakati kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga zinaendelea na hatimaye uchaguzi kuisha, kulitokea taarifa nyingi sana za mauaji ambayo yalihusishwa na siasa - Mauaji yaliyotolewa taarifa ni yale ya wanachama wa CHADEMA waliouawa katika mazingira tofauti huko. Mmoja alikuwa ni kijana, Mkazi wa Ubungo Dar es Salaam aliyeenda Igunga kusaidia uangalizi wa Vituo vya Kupigia kura na mwingine alikuwa ni mwanamke mwanachama wa CHADEMA pia ambaye mwili wake uliokotwa porini siku chache baada ya uchaguzi, niliwahi andika taarifa hizo katika makala kadhaa ikiwa ni pamoja na hii: http://msbillegeya.blogspot.com/2011/10/mauaji-igunga-maiti-zaidi-zaokotwa.html
Sasa kumeibuka taarifa nyingine za mauaji ya kiongozi wa CHADEMA huko Arumeru Mashariki, jimbo ambalo CCM imelipoteza kwa CHADEMA katika uchaguzi mwingine mdogo hivi karibuni! Taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa kiongozi huyo wa CHADEMA alipigiwa na watu waliodai kuwa kuna wanachama wa CCM wamekihama chama hicho na wanataka wapewe kadi za CHADEMA, kumbe walikuwa ni wahalifu waliokuwa wanatafuta roho yake - na kwa mara nyingine mauaji hayo yakahusishwa na Tofauti za Kisiasa baina ya vyama vya siasa huko.
Wiki hii Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikatoa taarifa ya Wazi kwa waandishi wa habari kwamba kuna wanachama wake wapatao 15 ambao wameuawa au kushambuliwa katika matukio ya yanayohusishwa na siasa tangu mwaka jana! Mbaya zaidi, ikaonekana kwamba jesho la Polisi hakuna lilipowahi kuchukua hatua madhubuti za kufuatilia mauaji au mashambulizi hayo na kuwatia nguvuni waliohusika kuwashambulia wana CHADEMA hao!
Jambo hili likanifanya nijiulize iwapo mauaji na mashambulizi hayo ni ya kisiasa - ni nani (kwa maana ya chama anayeweza kuwa yuko nyuma yake)? Katika hali ya kisiasa Tanzania kwa sasa, ni wazi kwamba Upinzani mkubwa wa Vyama vya siasa upo kati ya CHADEMA na CCM. Na kwa Tanzania bara, kila mtu anafahamu kwambza ushindani baina ya vyama hivi viwili - kitaasisi na hata katika ngazi ya watu binafsi ni mkubwa sana! Jambo hili linaweza kuanza kutoa mwanga juu ya nani anaweza kuwa anahusika na mauaji hayi iwapo ni kweli ni ya kisiasa!
Mbunge wa CHADEMA, Highness, Alishambuliwa kwa Siraha |
CCM kama Chama tawala kimekuwa kikishutumiwa sana kwa Ufisadi - aidha kwa kuufanya chenyewe kama Chama au kwa Kuwalinda na Kuwatetea wanachama na viongozi wake waandamizi ambao wamekuwa wakifanya vitendo kama hivyo. Jambo hili limewafanya wananchi wengi sana kupoteza imani na matumaini kwa chama hicho na baadhi wakaamua kuondoa kabisa matumaini yao kwa vyama vya siasa, na wengine wakaamua kubadilisha vyama - hususan kwa kujiunga na CHADEMA.
Ni ukweli kwamba CCM tuliyokuwa tunaifahamu na kuitumainia wengi wetu kwamba ndiyo itakuja kulisaidia na kulikomboa taifa kutoka mikononi mwa maadui wakuu wa taifa - sio CCM hii inayoweza kuyafanya hayo tena! Sasa kama ni kweli CCM imeamua kupiga hatua nyingine ya mbele zaidi katika uovu na uhalifu - kutoka Ufisadi hadi Mauaji ya Wanachama na Viongozi wa Vyama vya Upinzani - tena kwa mauaji ya kikatili kama yaliyofanyika Igunga na Arumeru - basi ni wazi kuwa Chama hiki sio tu kwamba hakifai kuliongoza taifa - bali pia hakifai kabisa hata kuendelea kuwepo kama chama kilichosajiliwa!
Kwa Upande wa pili, hata kama CCM haihusiki moja kwa moja na Mauaji au mashambulizi hayo dhidi ya Viongozi na Wanachama wa CHADEMA, kama chama tawala, bado kinabeba dhamana ya mabo mbalimbali yanayotokea nchini, kwa raia wa nchi hii, HUSUSAN yale yanayotokea Kisiasa!
Lakini kama tuhuma hizo ni za kweli na zinakihusu aidha Chama cha Mapinduzi kama taasisi au Wanachama wake wanaofanya hivyo kwa maslahi ya chama, basi ni wakati Watanzania wakaanza kuangalia upya ushiriki wao katika siasa za Nchi na kufanya maamuzi ambayo kwa hakika ndiyo yatakuwa na faida na maendeleo kwa taifa - lakini kama sio hivyo - basi taifa hili na siasa zake tunaelekea kubaya sana!
...///
Blogu inajitambulisha kama ya siasa lakini ina mwelekeo wa itikadi!
ReplyDeleteNamkubali mwenye Mbwa bali mbwa mwenyewe tayari keshajua nani atamngáta na nanni hatamngáta! Napata shida kujiunga
Umesema "Blogu inajitambulisha kama ya siasa lakini ina mwelekeo wa itikadi!", una maana gani? Maana Siasa yenyewe ni Itikadi, au wewe una maanisha nini?... maoni yako yanaweza kusaidia kurekebisha patakapoonekana hapajanyooka katika Blogu hii! Karibu
ReplyDelete