John Mnyika (Mb) |
Hukumu ya Kesi ya Kupinga matokeo ya Ubunge katika jimbo la Ubungo, Dar es Salaam ya mwaka 2010 ambapo Mbunge wa CHADEMA, John Mnyika alishinda inatarajiwa kusomwa kesho tarehe 24 Mei 2012 katika Jengo la Mahakama Kuu (Kivukoni) kuanzia Saa Nne Asubuhi.
Mbunge wa Jimbo hilo John Mnyika anawaalika wapiga kura wake wote na wananchi wapenda maendeleo kwa ujumla kuhudhuria Mahakamani hapo Mapema kwa ajili ya kusikiliza usomwaji wa hukumu hiyo. Hapa Chini ni Nukuu ya Taarifa ya Mbunge huyo kuhusiana na kusomwa kwa hukumu ya kesi hiyo:
"Nimepokea taarifa kwamba hukumu ya kesi ya uchaguzi dhidi ya ushindi wetu Jimbo la Ubungo kesho tarehe 24 Mei 2012 itatolewa katika Jengo la MAHAKAMA KUU (KIVUKONI-COURT No. 1) badala ya jengo ilipo mahakama ya kazi (akiba) ambapo kesi iliendeshwa. Kama tulivyotafuta kura pamoja, tukapanga mstari kupiga kura pamoja na tukakesha kuzilinda pamoja tujumuike pamoja kujua hatma ya kura zetu. Hukumu ya kesi inatarajiwa kuanza kusomwa SAA NNE ASUBUHI hata hivyo ni muhimu kuwahi mapema zaidi asubuhi kwa ajili ya itifaki za kuingia mahakamani.
MUHIMU: Mpe taarifa mwenzako!" John Mnyika (Mb)
Maslahi ya Umma kwanza!
No comments:
Post a Comment