John Mnyika, Mbunge wa Ubungo! |
Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mh. John Mnyika (CHADEMA) ameshinda kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa mwaka 2010 ambayo yalimpatia Ushindi dhidi ya mgombea wa CCM - Hawa Nghumbi - ambaye ndiye mlalamikaji katika Kesi hiyo.
Jopo la majaji limetupilia mbali hoja zote za kupinga matokeo hayo ambazo zilikuwa zifuatazo:
1) Kwamba Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za UWT
2) Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
3) Kuingia watu wengi wa CHADEMA ktk chumba cha kuhesabia kura
4) Kuzidi kwa kura hewa 16,000
5) Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form)
2) Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
3) Kuingia watu wengi wa CHADEMA ktk chumba cha kuhesabia kura
4) Kuzidi kwa kura hewa 16,000
5) Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form)
Mashtaka yote yametupiliwa mbali kwa sababu mbali mbali zikiwemo walalamikaji kutokuwasilisha kwa ushahidi, walalamikaji kutokuwepo katika maeneo ya matukio waliyokuwa wanayalalamikia.
Mlalamikaji, Hawa Nghumbi (CCM) ametakiwa kulipa gharama za kesi kwa kuwa ameshindwa!
hapa naona kwa mara nyingine tena mahakama imetoa haki kwa mnyonge. kama ingelikuwa ikifanya hivyo katika mashauri yote yanayofanyika basi demokrasia na maendeleo ktika tanzania tungefaidika nayo. hongera sana mtu wa watu-mnyika, john.
ReplyDeletemmm inawezekana wamelazimika kutoa haki hiyo maana waliforesee kitakachotokea kama wangefanya vinginevyo
ReplyDelete