Wiki iliyopita Rais Kikwete litangaza baraza jipya la Mawaziri, likiwa na sura nyingi za zamani. Maamuzi haya yalitokana na shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi wengi na wabunge wa vyama mbalimbali wakiwemo wa chama anachokiongoza yeye mwenyewe!
Janeth Mbene, Naibu "mpya" wa Waziri wa Fedha |
Wakati mabadiliko haya yanaweza kumaanisha kuwa yanatakiwa mabadiliko, swali linabaki, uongozi wa nchi hii unaweza kubadilika kwa kubadilishwa kwa baraza la mawaziri kwa "lazima" wakati Rais bado ni Kikwete huyo huyo?
Kuchelewa kwa Kikwete kufanya maamuzi ambayo ni wazi kuwa yalitakiwa kufanyika zamani, na kitendo cha yeye kutoyafanya mpaka alipotishiwa na wabunge hadi wa chama chake mwenyewe kuwa wangeiangusha serikali yake nzima iwapo asingefanya maamuzi inaacha maswali kadhaa ya msingi. Baadhi ya maswali ni pamoja na haya:
KWANZA: Je, Rais mwenyewe anaamini kwamba mabadiliko aliyoyafanya yalikuwa ni ya lazima kufanyika au ameyafanya ili kuwaridhisha waliokuwa wanayataka - japo alijitahidi siku nyingi kuwapinga mpaka walipomshinda nguvu!
PILI: Je, Mawaziri hawa wapya wataweza kuboresha uharibifu mkubwa ambao umeshuhudiwa katika serikali na nchi hii tangu Kikwete alipoingia madarakani - wakati yeye akiwa bado yuko Madarakani?.. Pamoja na mengine mengi.
Wakati tunaendelea kusubiri kuona kama mawaziri hawa wapya wataweza kuleta mabadiliko tunayoyataka katika taifa, ni muhimu watanzania tukaendelea kujiuliza - nchi hii itakuwa ni ya kufanyiwa majaribio ya viongozi mpaka lini? Ni lini ambapo tutakuja kuweka viongozi wenye sifa na uwezo madarakani ambao hawatupotezewa miaka mingi ya kusubiri kuwapa muda wafanye wanayoyafanya mpaka tunapokuja kubaini madudu na uozo waliokuwa wanaufunika?..
Wakati tukiendelea kusubiri kuona iwapo hawa watakuwa tofauti na waliowatangulia, nashauri tuutumie huu muda kujiandaa kwa kuwatambua watu wanaofaa kuliongoza hili taifa tangu sasa na tuwachague hao katika uchaguzi mkuu ujao - tusiendelee kuliweka taifa letu mikononi mwa watu "wanaojaribu" kuongoza tena, tuwape watakaoweza kuifanya hiyo kazi. Orodha ya Wizara, Mawaziri na Manaibu wao hii hapa chini!
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU
MAWAZIRI
MAWAZIRI
1. OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
(Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,
2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu,
Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya
P.L. Huvisa, Mb.,
3. OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,
4. WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa Ujenzi
Dr. John P.
Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii
Dr. Hussein
A.H. Mwinyi, Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi
Dr. Shukuru J.
Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe,
Mb.,
Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo
na Uvuvi
Dr. David M.
David, Mb.,
Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka,
Mb.,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia
Prof. Makame M.
Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna K.
Tibaijuka, Mb.,
Waziri wa Maji
Prof. Jumanne
Maghembe, Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara
Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,
Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika
Eng.
Christopher Chiza, Mb.,
Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E.
Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah
O. Kigoda, Mb.,
Waziri wa Fedha
Dr. William
Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter
Muhongo, Mb.,
5. NAIBU MAWAZIRI
OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI
6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu
wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,
7. OFISI YA WAZIRI MKUU
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa,
Mb.,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,
8. WIZARA MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro
M. Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro,
Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye,
Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,
Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla
Juma Abdulla, Mb.,
Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu,
Mb.,
Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi
wa Jamii,
Dr. Seif
Suleiman Rashid, Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na
Madini
Ndugu George Simbachawene,
Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J.
Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,
Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith
Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki,
Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
What you havе written in "MAWAZIRI Wapya: Wataleta Mabadiliko Chini ya Kikwete Huyu Huyu?" is definitely not totаlly onlу grеat
ReplyDeletebut аctually mοԁel of impоrtаnt.
I know a number of people don't really keep in mind these products. But once you offer a similar experience to me and are sorted out losing weight or dependency or from associated with the the things you truly can thinking about I usually tend to appreciate what I read as it is really the actual easiest way to gain in knowledge with out actually doing the things. On this reason I enjoy finding out different peoples aspects of views and experience.
Have a look at my weblog: 5htp.org
My site: 5htp.org